Huu ni upendo, utu wema au mtego?

Huu ni upendo, utu wema au mtego?

Nilikwenda mahali kupata huduma.

Aliyenipokea ambaye baadae nikaja jua kua ni mmiliki ni dada mmoja mrembo tu.

Wakati naweka oda yangu tulipata wasaa wa kuzungumza kidogo.

Nikapewa muda wa kwenda kuchukua bidhaa yangu.

Sasa wakati wa kuichukua nikaona movements ambazo sizielewi na pia sura yake ili badilika kidogo mara moja nikahisi kutakua na tatizo.

Akaja pale na ile bidhaa yangu akaomba radhi na pia akanipa muda wa kuja kuichukua tena ikiwa imefanyiwa marekebisho.

Siku nafika pale naikuta bidhaa yangu ipo sawa kama nilivyoagiza na akaandaa na nyingine tena kama ile.

Kwakweli nilishangazwa maana kwa maisha ya sasa wema ule ulinishtua.

Nikawa nawaza, huu ni mtego?? Wema wake?? Au labda ni upendo wa kuhitaji mahusiano ??

Nilichukua kadi yake lakini nasita kumtafuta.
CCM hamuaminiani.Hata maji ya kunywa mtu wa CCM akikupa usinywe.😂😂
 
Akili za vijana wa UVCCM bana, hasara tupu.
 
Man!! She is doing her work, trying to retain customers like you and you are here wondering customer service you have received.
Collect yourself hiyo ni kawaida Tu au unataka tukwambie anakutaka?
 
Mi nliwahi penda cadet kwa duka la mrembo fulani,ikaw ndogo nikaomba anitaftie ya namna ile lakini saizi yangu, ilichukua cku kuipata ko nlipata ka mara mbili tatu ivi, cku alivyoipata alinipatia hiyo cadet na staff jeans mpya, by the time ckuwa navaa staff jeans, na mimi ukarmu ule ckuelewa na nlivyoenda uliza bei nikaambiwa 38,na nguoa nliyonunua ni 28 nikashindwa elewa, bt in future I went back and bought 3 of them kutoka dukani kwake.. it's business tactics
episode ikaishia hapo hapo??
 
Man!! She is doing her work, trying to retain customers like you and you are here wondering customer service you have received.
Collect yourself hiyo ni kawaida Tu au unataka tukwambie anakutaka?
Dunia imebadilika sana mkuu

Kitendo kimoja tu unaweza jikuta kwenye situation ambayo hukutarajia kabisa.
 
Ambacho umesahau ni kwamba mara ya kwanza ulikuta bidhaa ina mapungufu, hilo ni doa kwenye biashara yake.

Ukaondoka na kurudi siku nyingine; hapo umepoteza muda na gharama za usafiri. Amefidia kwa kukupa bidhaa ya nyongeza ili uendelee kuwa mteja wake. Hiyo ni akili ya biashara.

Hata hivyo kuna watu wamepata wapenzi, wengine wakapata mpaka mke kupitia biashara kama hivyo. Inaonekana kabisa yeye amekuhudumia vizuri kama mteja tu, lakini hilo halikuzuii wewe kumtongoza. Au unataka mseleleko..!
 
Wabongo aisee!!!

Siku za nyuma kuna abiria mmoja kutokea Bongo aliingia matatizoni baada ya kulazimisha busu na kumbato(hug) kutoka kwa air hostess wa ndege ya Emirates iliyokua ikienda Marekani

Jamaa alielewa vibaya kule kuchekewa chekewa na air hostess kua labda demu kamzimia asielewe yale ndio mahitaji ya kazi yao na wapo hivyo kwa abiria wao wote[emoji23][emoji23][emoji23]

Kama umemuelewa basi fata procedures za kummiliki(umtongoze). Kutegemea kua amekupenda wewe kwa sababu ulizozitaja, kwa maoni yangu sio sahihi
 
  • Kicheko
Reactions: amu
Back
Top Bottom