Huu ni Utapeli au ndivyo Biashara inavyofanywa?

Boss Man

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2022
Posts
458
Reaction score
991
Wajuzi mnaonunua magari mara kwa mara naomba uzoefu wenu hasa mnaonunua magari mikononi kwa watu

Leo Kuna Gari nilikuwa nataka kununua kwa mtu lakini Dalali kaja na mtu anayedai ni mmiliki wa hiyo Gari lakini Cha ajabu Majina yake hayapo kwenye kadi ya Gari anadai hakufanya transfer

Sasa Wakati tunataka kufanya Biashara wakadai issue ya Majina Haina tabu kwamba wao niwape Chao then Mimi kwa muda wangu nitaenda TRA kufanya transfer ya Majina bila mmiliki wa mwanzo kuwepo.

Sasa swali lipo hapo, inawezekana kufanya transfer ya Majina kwenye kadi ya Gari bila mmiliki kuwepo?
 
Usikubali na hakikisha mwenye jina umempata na pia kadi original uione, utaratibu ni lazima upate kitambulisho cha mwenye jina kiwe cha taifa au leseni, cha kura na picha passport size, mkataba wa mauziano pia.

Usikubali kununua gari bila kumpata muhusika mwenye jina na ukiuza gari usikubali jina lako liendelee kutumika huko gari inapokwenda, kuwa makini sana na gari iliyopita mikono zaidi ya miwili au mmoja bila kubadilishwa jina la muhusika.
 
Utaingizwa mjini na wajanja huwezi kufanya transfer ya gari bila kitambulisho cha mwenye gari mkataba wa mauziano tena uonyeshe majina ya mwenye gari yanayosoma kwenye kadi ya gari na pia uwe na muhuri wa mwanasheria pia mkataba ulipiwe kodi

Angalizo usije kuuziwa gari ya wizi
 
Duuu mazingaombwe kumbe yanaendelea Huko mtaani...
Wajanja wanataka KUKUOGESHA NA NGUO ZAKO
 
Shukrani mkuu kwa muongozo....Iko hivi, huyu anayetaka kuniuzia Gari Majina yake hayasomi kwenye kadi ila amekuja na kopi ya kitambulisho Cha mhusika wa Hilo gari ambalo amedai kalinunua kutoka kwake

Wenyewe wanadai kuwa wakinunua Magari kwaajili ya kufanya Biashara huwa hawabadilishi Majina kadi wanaiacha kama ilivyo, Sasa wakishapata mteja ndio wanamshauri ku transfer Majina...hapo ndio nilitaka kujua kwamba hizi Biashara zinafanyikaga hivi au ni ujanja ujanja tu?
 

Pia hata kama mwenye gari hayupo karibu
Lazima TRA watampigia simu kuhakikisha kabla ya Transfer (Maana kuna zile transfer za juu kwa juu bila wamiliki wote kufika ofisi za TRA)
Ila lazima wampigie Simu kuhakikisha na kumnulisha kuwa gari linabadilisha umiliki (Kama simu yake kipindi anajisajili haipatikani lazima aje mwenyewe)
 
Hivyo vyote jamaa kaja navyo, kitambulisho Cha huyo aliyekuwa mmiliki wa Hilo gari, Kadi OG, so nilitaka kujua kwamba kama TRA wanaweza kufanya transfer ya Majina kwa kopi ya kitambulisho tu bila mwenye kitambulisho chake kuwepo (ambaye ndiye aliyekuwa akimiliki gari)


Mfn: wewe unipe Kadi ya Gari lako pamoja na kopi ya kitambulisho nikifika TRA naweza kufanya Transfer ya Majina kuja kwangu bila wewe kuwepo?
 
Hilo ni ķanjanja mjomba, huwezi kufanya transfer bila mmiliki wa gari kuwepo, hata kama kuna ukweli wa jambo hilo basi ni bora mukutane ana kwa ana na huyo mmiliki ili mukubaliane kwamba atakuwa tayari kukusaidia jambo hilo.

Sent from my SM-A530N using JamiiForums mobile app
 
Huyo ni dalali mjanja mjanja...tafuta dalali anaejua kazi hiyo...TRA wanataka kitambulisho cha mwenye gari, we unacho? unamjua? passport picture ya mwenye gari unayo?
 
Inawezekana kwa sisi wazoefu ila kwa mgeni wewe usijaribu utapigwa.
 
Huyo ni dalali mjanja mjanja...tafuta dalali anaejua kazi hiyo...TRA wanataka kitambulisho cha mwenye gari, we unacho? unamjua? passport picture ya mwenye gari unayo?
Ndio kitambulisho kipo, Dalali amekuja nacho, na Kadi anayo ila mwenye gari hayupo
 
Ndio kitambulisho kipo, Dalali amekuja nacho, na Kadi anayo ila mwenye gari hayupo
Kama umeshanunua tafuta watu wataibadilisha, kama bado hujanunua nenda mwenyewe TRA
 
Kikubwa iwepo ID ya mwenye Gari yenye jina linalofanana na la kwenye Kadi. yaweza kuwa Passport au kitambulisho cha uraia na mkataba wa mauziano. Mambo mengine uwe unawapa watu wa kufanyie. ukileta usomi na complications za usomi utachelewesha zoezi.
 
Mkuu kwa kuwa umeshapata mashaka na jambo hilo isikilize nafsi yako kitu inachotaka ufanye.

Mimi kwa ushauri naomba ufanye mpango huyo muhusika awepo kwenye transfer, nakupa mfano huenda huyo mwenye gari alikopo kwa huyo muuzaji wako na bado wapo kwenye mkataba ujue siku wakimalizana atahitaji gari yake huku na wewe ulishauziwa hapo mtapoteza muda na usuluhishi ambao huku awali unaweza kuuepusha.

Usifanye kwa kuwa wengi wanasema unaweza kufanya ila fanya kwa kufata utaratibu ili usije kujiingiza kwenye matatizo.

Binafsi najua ninachokisema hapa tulishateseka sana na mauziano ya kienyeji kama hayo mtu kauza gari kumbe ana mkopo benki wanalitafuta hilo gari na kadi og jamaa alikuwa anayo hapo sasa ndio utajua umuhimu wa kwenda kuhakiki na muhusika kamili.
 
Angalia hii thread yale tunayokushauri uyakwepe ndio yamemkuta jamaa


 
Mkuu huyo mwenye gari sio lazima awepo ila hakikiaha una passport size picha zake namba ya simu na kitambulisho chenye jina sawa na jina la kwenye kadi. Lakini sababu una mashaka fanya naye mazungumzo kabisa huyo mwenye jina kwenye kadi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…