Ni hivi yalimtokea shost, boyfriend anakwenda kwake, lakini hamfahamishi nyumbani. Mpaka wamepata mtoto, mama mkwe amekuja kumwona mtoto, ubatizo wa mtoto umefanyika kwa shost mama amekuja kama mgeni. Sasa siku moja shost anakwenda Kariakoo shopping, anakutana na jamaa yuko na mother, khe, baada ya salamu aliuliza mnakwenda wapi, mama alijibu kupanda basi twende nyumbani, mama alikuwa na mzigo, shost aliofer lift, jamaa alitaka kutoa nje, mama aliona unafuu ule alikubali.
Wamefika home, masikini mama anaishi kwenye nyumba ya nyuma mbele ameweka msingi tu na ni wa muda mrefu. shost aligundua kwanini jamaa alikuwa hataki afike home. Sasa kama mtu umesha zaa nae, haya si ni mambo ya kawaida tu. Hakuna aliyeumbiwa umasikini.