Huu ni uwongo wa mchana kweupe, nakataa katakata

Huu ni uwongo wa mchana kweupe, nakataa katakata

Pettymagambo

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2017
Posts
1,490
Reaction score
8,227
Mojo kwa moja kwenye mada"

Kumekuwa na takwimu inasambazwa kwenye magroup mbalimbali ya michezo eti Mnyama mkali kuliko wote mwituni ndie anaongoza kwa kupiga pasi nyingi.

Mimi kama mwana simba nasema huo ni uwongo wa kutaka kubalance mambo hasa baada ya kuonekana haya majamaa {utopolo} yanaupiga mwingi mpaka unamwagikia.

Tumeona wote namna timu pinzani zinavyoteseka tangu sekunde ya kwanza mpaka ya mwisho, eti leo mtu anakuja na vitakwimu simba anaongoza kwa passes? Sote tunaona mpira wetu ambavyo umekuwa wa mashaka japo tunashinda, ila kusema tumewazidi passes uto?

Hili ni hapana, nipo tayari kutukanwa na kuitwa uto mteule, ila ukweli yale majamaa yanatisha haki!
 
Unajipiga dole na kujinusa mwenyewe.

Unakataa huku huna data. Linganisha data zinazozunguka mtaani na zako unazodhani ni sahihi.

Vinginevyo acha porojo.
 
Mechi ya namungo yanga alicheza kawaida sna.. na mechi ya simba vs coasta hata kama simba hakucheza vzr kama mnavo dai ila alipiga pass karibia 80% zilizokamilika.
 
Ninakuja na software na mfumo wa kisasa itakayotumika kukusanya data zote za viwanjani na kuzichakata na kuzihifadhi nafikiria itasaidia sana kuondoa ubishi kama huu, taarifa kuonekana live kila baada ya dakika 45 za michezo yote ya ligi kuu 🤝, ligi yetu aifai kuwa namba tano ni uongo tu ata taarifa muhimu za mechi zinakusanywa kienyeji
 
Unajipiga dole na kujinusa mwenyewe.

Unakataa huku huna data. Linganisha data zinazozunguka mtaani na zako unazodhani ni sahihi.

Vinginevyo acha porojo.
Mkuu kulikuwa hakuna haja ya kutumia maneno ya karaha hivyo ilihali mleta uzi kawasilisha tu mawazo yake ambayo hayawezi kuwa sawa sawa na mitazamo ya kila mtu.

Tukija kwenye mada, tukiangalia aina ya mpira anaocheza Simba na anaocheza Yanga msimu huu ni aina mbili tofauti. Mpira wa Yanga ni mpira ambao wanacheza kwa mfumo wa kuanzia mashambulizi kwanzia golini kwao kwenda hadi golini kwa mpinzani na pia wamekuwa watu wa kuhakikisha wana win mpira kwa haraka pindi mpira wakipoteza. Hii maanake ndio timu inayohakikisha wanakaa na mpira muda mwingi kuliko mpinzani na obvious lazima upande wa pass zitakuwa ni nyingi

Tukiangalia aina ya mpira wa kocha wa Simba, sio muumini wa kucheza mpira wa pasi nyingi lakini ukiachana tu na hilo ni kwamba wachezaji wa Simba wana accuracy ndogo sana ya utoaji wa pasi, mara nyingi pasi zao hupotea. Kuna watu kibao wamelalamika juu ya wachezaji wa Simba kushindwa kufikisha hata pasi 10 pasipo kupoteza mpira, hadi kuna wadau wamekuja na uzi wa mazoezi ya Rondo kwa wachezaji wa Simba hiyo yote ni kutokana na kuonekana wazi kuwa wachezaji wanashindwa kupasiana pasi nyingi pasipo kupoteza mipira. Hili nakupa hata wewe kazi ya kwenda kuliangalia kwanzia mechi ya za mzunguko wa kwanza hadi wa tatu kwa Simba na Yanga embu tazama control ya wachezaji, accuracy ya pasi na spirit ya wachezaji kati ya Simba na Yanga utakuja kupata jibu. Spirit, accuracy na ball control za wachezaji ndio zitakazozalisha wingi wa pass.

Mpira ni mchezo wa wazi mkuu, kila kitu kinaonekana hivyo hakufanyi ushindwe kuona uongo wa takwimu hata kama hauna data.
 
Mpira unachezwa hadharani, sote twaona wananchi wanavyoupiga mpira mwingi na passes lundo, tukana matusi yote ila yanga wametuzidi mbali!
Upo sahihi Baba Yunge japo wana lunyasi wenzio wanakupomda. Sijui kwanini sasa vijana mnafanyana wajinga alafu yule msemaji wa Simba anawadharau sana wanasimba. Ukifuatilia mpira kwa sasa kati ya Simba na yanga. Ni kujitoa akili tu Simba kujifananisha na Yanga otherwise Natoa cement ya kujenga sanamu la Rage pale Msimbazi.
 
Yaani unabuniwa uwongo tu na mtu mmoja, then unaletwa kwenye magroup, nasi tunadandia hivyohivyo na kuanza kutamba na takwimu za kipuuzi japo ukweli upo wazi!
 
Mojo kwa moja kwenye mada"

Kumekuwa na takwimu inasambazwa kwenye magroup mbalimbali ya michezo eti Mnyama mkali kuliko wote mwituni ndie anaongoza kwa kupiga pasi nyingi.

Mimi kama mwana simba nasema huo ni uwongo wa kutaka kubalance mambo hasa baada ya kuonekana haya majamaa {utopolo} yanaupiga mwingi mpaka unamwagikia.

Tumeona wote namna timu pinzani zinavyoteseka tangu sekunde ya kwanza mpaka ya mwisho, eti leo mtu anakuja na vitakwimu simba anaongoza kwa passes? Sote tunaona mpira wetu ambavyo umekuwa wa mashaka japo tunashinda, ila kusema tumewazidi passes uto?

Hili ni hapana, nipo tayari kutukanwa na kuitwa uto mteule, ila ukweli yale majamaa yanatisha haki!
Ni mbinu nzuri sana hiyo nimeipenda. Ukiwa unaonekana ni mgonjwa huku watu wanakusifia upo imara na shupavu, maanake wanataka usitibu ugonjwa ili ufe. Aliyeanzisha hiyo propaganda inawezekana anataka kuziba kelele za mashabiki wanaohoji juu ya aina ya soka linalotandazwa msimu huu.
 
Simba Ilikuwa inapiga pass miaka Ile.

6. Thadeo Lwanga. ( Hapotezi mpira dk 90)

7. Luis Miquisson.
8. Jonas Mkude.
9. Chris MUGALU
10. Clotas Chama
11. Rary Bwalya.

Simba Haina Tena wachezaji kama Hawa
Amebaki chama Peke yake.

Muzamiru kanute na KIBU ndio wachezaji wanaoongoza kwa kupiga pass fyongo na KUPOTEZA MIPIRA.
 
Sawa, kwahio nawe pia unakubali hizo takwimu za kubumba sio za kweli na zimetengenezwa ili kuzima kelele za wapinzani wetu kuwa na taqwimu bora kutuzidi katika kila kitu isipokuwa topscorel?
 
Back
Top Bottom