Babu Kijiwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2010
- 4,845
- 4,776
Habari zenu,
Kwa muda mrefu sana msajili wa vyama vya siasa amekuwa akivibeba vyama vya upinzani hasa CHADEMA pale vinapovunja kanuni, taratibu na sheria za nchi. Sijajua kuna nini nyuma ya pazia ila sasa ni wakati muafaka wa kukifuta Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Wiki hii jeshi la polisi lilitoa tahadhari kuhusu mikusanyiko isiyo rasmi na lilithibitisha kuwa halijajulishwa uwepo wa mkusanyiko wowote unao husiana na mapokezi ya kiongozi wa upinzani aliyetoroka jimbo.
Chakushangaza leo CHADEMA wamekusanyika, wameandamana na hii ni kinyume kabisa na sheria zetu kwani hawajapewa kibali cha kufanya hivyo.
Tafadhali sana msajili wa vyama vya siasa nakuomba sana KESHO UKIFUNGIE CHAMA HIKI MILELE ili tuendelee kudumisha amani na upendo nchini vinginevyo kitatuletea machafuko yasiyo na lazima.