Huu ni wakati wa Rais Samia kuisuka upya Serikali yake, hujuma zimeanza kuwa za waziwazi

Huu ni wakati wa Rais Samia kuisuka upya Serikali yake, hujuma zimeanza kuwa za waziwazi

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Leo nimeenda kununua umeme kituo kimoja cha TANESCO.

Nikiwa kituoni pale kulikuwa na msururu mrefu sana wa wananchi wakiwa kwenye foleni, akaja mtu ambaye haiba yake inaonyesha ni mtu mwenye uwezo hivi kifedha. Yule bwana akajinadi kuwa ni Muinjilisti, akaanza kuchanganya maneno ya dini na siasa kwa staili ya kuwahubiria watu, akaanza kumponda rais Samia kuwa anadanganywa n. k

Huyu bwana pia aliingia ndani ya geti na kuanza kufanya mahubiri ya kumponda raisi Samia lakini wakati huohuo akichanganya na kumtaja Mungu

Nikatafakari sana tukio hilo, nikatafakari choice ya location ya mahubiri yake ya kisiasa, Kwa nini amekuja eneo lile ambalo watu wana frustrations za umeme kutopatikana. Je, huyu mtu alitaka kucapitalize kwenye kero hii ya umeme ili kupenyeza sumu ya kuwataka watu wamchukie rais?

Kiufupi binafsi ninahisi something haiko sawa, kuna haja ya Rais Samia kupanga safu yake ya uongozi. Kuna Loyalist wa Magufuli ndani ya serikali yake ambao hawaamini kuwa masilahi yao na priviledges walizokuwa wakizipata enzi za Magufuli wataendelea kuzipata!

Hili kundi linajaribu kumblackmail rais Samia kuwa wanaweza kumharibia.

Hili kundi lilikuwa shocked kutokana na kifo cha rais Magufuli, initially walikuwa in denial, sasa wapo kwenye phase ya Hasira, Rais Samia inabidi alisaidie hili kundi lije kwenye acceptance stage haraka, na njia nzuri ya kufanya hivyo ni kufanya purging ya wale vinara ili wale dagaa waliobaki waje kwenye compromising stage.

Kuharibika kwa hii mifumo ya taasisi nyeti tena zinazohusu collection ya fedha haiwezekani ikawa ni coincidence tu, hata kama ni coincidence ni muhimu watu tena wakubwa wawajibishwe ili kutuma meseji kali kuwa hii kitu haivumiliki na haikubaliki.

Raisi alifanya recycling ya baraza la Mawaziri, japo hiyo move ililenga kutuliza taharuki katika utendaji wa serikali, lakini ipo haja ya kuliunda upya baraza la mawaziri ili iwepo total loyalty kwa rais Samia.

Hivi sasa wateuliwa kwa sababu ni zao la Magufuli wana divided loyalty, moja kwa hayati na ya pili kwa Samia. Sasa Samia hana budi afikirie kuunda upya baraza lake, na akiunda jipya aangalie asiingie katika mtego wa kuwaingiza kundini wale "chawa" wa hayati, atafute watu wake!
 
Leo nimefarijika sana na maneno ya spika wetu mpendwa wa bunge la JMT Mh. Job Ndugai pale aliposema; nanukuu "rais ni mmoja tu aitwaye Mh. Samia Suluhu Hassan na hakuna marais wa wilaya wala mikoa.

Hakika cheo cha urais kinatisha mno hususani zile nguvu alizopewa na katiba (presidential decree)

Nguvu hizo ni nguvu kuntu walizomkabidhi Watanzania ili taifa letu lisonge mbele kiutulivu na kimaendeleo.

Hakika cheo chake kinatisha mno. Huwa ninashangaa kuona Mtanzania anampinga rais kwa maneno makali tena ya argumentum ad hominem khaaaaa

Nijuavyo rais anaweza kukosolewa kwa staha na maneno ya heshima.

Rais ni zaidi ya wazazi wetu na watu wengine tunaowaheshimu.

#Staunchsupporterofssh
 
Acha ramli zisizokuwa na maana. samia abadilike yeye kwanza, anatakiwa awe mkali asitake kupendwa na kila mtu. akienda na mwendo huu, hata akimuweka nani hakuna kitu. Enzi za JPM watu aliowaweka sio wote walikuwa wanamkubali ila walikuwa wanamuogopa hata kujaribu tu kufanya hujuma. Mama anadilike hii nchi ina mambo mengi sana.
 
Ishu sio watu wa Magufuli, au kuhujumiwa. Ishu ni kwamba Mama anacheza too low. Nilishangaa hata ziara ya Waziri Mkuu bandarini, amekuwa mpole, alienda hana clue yoyote na aliishia kudanganywa.

Mpaka sasa Mama ameshaweka watu wake sehemu nyeti, acheni kupiga porojo kwamba anahujumiwa.

Mfumo wa mitandao/malipo wa serikali (eGA) kaweka mtu wake.
TCRA kaweka mtu wake
Katibu Mkuu kiongozi kaweka mtu wake
PCCB kaweka mtu wake
TRA kaweka mtu wake
TPA (BANDARINI) kaweka mtu wake
Katibu Mkuu Wizara ya fedha kaweka mtu wake
Katibu wa Bunge kaweka mtu wake
Waziri wa TAMISEMI kaweka mtu wake
UDART kaweka mtu wake

Hata huko CCM ameshapangua safu za Hayati.

Shida ya Mama ipo ktk kusimamia kila anachokisema.
 
Oohh please, feed this rubbish to the pigs!

Umesema kwamba Rais anatisha sana?

Labda, inawezekana!

Lakini kwa BIBI KIZEE huyu!!!! Sidhani.

Yeye mwenyewe hajiamini kama ni Rais.

Hata ukimuuliza atakwambia yeye ni "Rais mwenye jinsia ya kike"!
Nawe ni miongoni mwa watu wenye kukosa ADABU NA STAHA.

Huiheshimu katiba adhimu nchi iliyompa mamlaka hayo makubwa?

Unamuangalia Kama mtu unayependa kumtafsiri UFURAHISHAVYO NAFSI YAKO na si KITI CHAKE?

Narudia kuandika, ndio RAIS ANATISHA.

Anatisha kwa kuwa UTULIVU WA KITI CHAKE ndio UTULIVU wa nchi na utulivu wa wanasiasa WEREVU na wale mahoka.

Mh.Rais Samia anajiamini na ametonesha KUJIAMINI huko kwa dhahabu kwa MUDA MFUPI MNO.

Unataka akuoneshe KUJIAMINI usemako kwa yeye kufanya nini?

Tatizo mnaishi kwa kukariri mno.
 
Vipi kama kuna kundi jingine ambalo si la Magu ambalo nalo linataka kuonyesha kuwa kuwa mama anahujumiwa na watu wa Magu ili lijipatie uhalali kwa kuwahujumu wanaodhaniwa kundi la Magu? siasa ni mchezo wa mahesabu na maslahi ya nchi huwa ni maslahi ya watu na watu ndo wana yapambania kwa mbinu mbalimbali uongo ufitini NK. Kalemani ajiangalie nadhani hivi karibuni atasaidiwa.
 
Acha ramli zisizokuwa na maana. samia abadilike yeye kwanza, anatakiwa awe mkali asitake kupendwa na kila mtu. akienda na mwendo huu, hata akimuweka nani hakuna kitu. enzi za JPM watu aliowaweka sio wote walikuwa wanamkubali ila walikuwa wanamuogopa hata kujaribu tu kufanya hujuma. mama anadilike hii nchi ina mambo mengi sana.
Kwa hiyo rais mzuri ni yule mwenye KUOGOPWAOGOPWA kikoko?

Hapa TUTAFAKARI, sidhani Kama Kuna mtanzania asiyemheshimu mh.Rais.

Mh. Rais Samia Suluhu Hassan si mtu wa maneno mengi.

Na viongozi wasio na maneno mengi HADHARANI huyafanya mengi makubwa.

Tatizo mmejikaririsha.

Hata STYLE ya utawala wa BABU YAKO na nyumba yake si sawa na wa MWANAYE ambaye ni baba yako ijapokuwa WOTE WANATIIWA NA KUTIISHA NIDHAMU.
 
Vipi kama kuna kundi jingine ambalo si la Magu ambalo nalo linataka kuonyesha kuwa kuwa mama anahujumiwa na watu wa Magu ili lijipatie uhalali kwa kuwahujumu wanaodhaniwa kundi la Magu? siasa ni mchezo wa mahesabu na maslahi ya nchi huwa ni maslahi ya watu na watu ndo wana yapambania kwa mbinu mbalimbali uongo ufitini NK. Kalemani ajiangalie nadhani hivi karibuni atasaidiwa.
Word and on Point...

Makundi ambayo 'sit on the fence' ndo hatari kabisa....
 
Back
Top Bottom