BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Mdogo wangu kaniajia ana matatizo katika ndoa yake waliyofunga miaka nane iliyopita. Anasema liwalo na liwe hata kama ni kuvunja ndoa hiyo ivunjike kama mkewe hatafuata utaratibu wake.
Hawa wanandoa wana duka ambalo mkewe ndio anasimamia. Siku za karibuni mkewe ameanza tabia akifunga duka saa 12 jioni anapitia bar na marafiki zake wanapata mbili tatu bia ndio anarudi nyumbani - hata saa tatu mpaka tano usiku. Jamaa amemind na kumtaka aache mtindo huo na bibie nae kaja juu ati yeye sio mtoto mdogo kwani hafanyi chochote kibaya anapokua na marafiki zake. Siku hizi hata akumwambia ampitie wakati wa kurudi nyumbani mkewe hataki hivyo jamaa anahisi mapenzi yamepungua au yamehama.
Sasa jamaa anasema amechoka na tabia hii na anatake achukue hatua yoyote hata kama ndoa itavunjika basi kieleweke kwani haoni raha kuwa na mke asiyempa kampani.
Kabla sijamshauri la kufanya naomba mawazo yenu wana JF, mnaionaje hii ni wivu tu wa jamaa au bibie anaweza kuwa na lake jambo?
Masikilizano ndani ya nyumba ni muhimu ili kuendelea na ndoa ya amani. Hii tabia na shemejio haikuwako miaka ya nyuma ni tabia ambyo ameanza hivi karibuni. Nakubaliana na mdogo wako kama mkewe hataki kubadilisha tabia yake ya kupita sehemu sehemu ili kupata moja moto moja baridi na hivyo kutomtii mumewe basi ndoa hii ina dosadi kubwa ambayo inaweza kusababisha kuvunjika kwa ndoa hiyo.