Zanzibar 2020 Huu sasa ni ufalme; haiwezekani watoto na familia ya Mwinyi iteuliwe kugombea kuanzia Urais hadi Ubunge

Zanzibar 2020 Huu sasa ni ufalme; haiwezekani watoto na familia ya Mwinyi iteuliwe kugombea kuanzia Urais hadi Ubunge

Mkakati ni kuwe na watu wa kuijenga hoja ya Baba yao ya kumuongezea miaka 5 ya shukrani.

Ndo mana nasema kuna kusudi maalum la Mungu kumponya Tundu Lissu zile risasi 16 na kumleta Tanzania mwaka huu!! Kuna ushenzi mkubwa sana ulikuwa unataka kufanyika Tanzania. Bora Mungu ameingilia kati kwa kweli!
 
Kwa nini familia ya Nyerere inatoswa sana na wajumbe wa Ccm na kwa nini familia ya Mwinyi imebebwa sana huko zanzibari na WAJUMBE?

NOTE;MODE USIFUTE UZI HUU.
Dingi yao hakua na hela/fisadi sasa watawa shawishi vipi wajumbe mkuu?
 
Hahaha Chadema kina wagombea, ACT inawagombea, wasiwasi wenu nini hao wakigombea?!

Siasa haina mwenyewe kuna wakati ni bahati, kama hamuwataki ni vizuri mkajadili watu mbadala wa vyama vingine.
Mnafahamu ccm ina wenyewe na wenyewe ndio hao.

Simamieni vyama vyenu yakwao waachieni, hiyo ndiyo demokrasia, muwakatae kwa kura.

Vyama visiposimamisha wagombea wazuri, hao msiowataka watashinda kweli.
 
WAJUMBE wa kamati ya STD VII, kuja huku, kuna watu wa kukata majina.
 
FRED lowassa
Salma Kikwete
Ridhiwani Kikwete
.....
.....
CCM INA WENYEWE. WENYEWE NDIO HAO. sisi kazi yetu ni kusema MITANO ZAIDI[emoji1787][emoji1787][emoji1787] ili waendelee kula mema ya nchi
Kuna mtoto wa Pinda,Mke wa Malecela
 
Mleta hii maada Lissu pamoja kelele zote hajui cdm ni chama ambacho muasisi ni Baba Mkwe wa mkt. Na akae akijua mwaka 2025 ya wezekana mgombea urais akawa mtoto wa mkt ambaye kesha anza mazoezi ya kisiasa kwa kutangaza nia ubunge Moshi mjini.
 
Mleta hii maada Lissu pamoja kelele zote hajui cdm ni chama ambacho muasisi ni Baba Mkwe wa mkt. Na akae akijua mwaka 2025 ya wezekana mgombea urais akawa mtoto wa mkt ambaye kesha anza mazoezi ya kisiasa kwa kutangaza nia ubunge moshi mjini
Lissu alikua bungeni na dada yake Christina lissu lakini ameyasahau,naona hoja zimeanza kumuishia.
 
Back
Top Bottom