Huu sasa ni wizi. Toka GB 1 kwa 1500 hadi 650 mb!

Huu sasa ni wizi. Toka GB 1 kwa 1500 hadi 650 mb!

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Huu ni uhuni wakuu, Tigo GB moja ilikuwa 1500. Wakaleta mb 900. Juzi zikawa 750. Leo kwa 1500 unapata Mb650. Kwa hesabu za uwiano, hiyo mb 650 ilitakiwa kuuzwa Tsh 975. Kuna Tsh 525 nzima tumeongezewa. yaani Bei imeongezeka kwa asilimia 53 ndani ya muda mfupi tu!.

Huu ni uhuni, ni bidhaa gani zinaongezeka bei kwa kasi kiasi hicho? Sasa wakuu, nini kudeal na uhuni huu wa mitandao ya simu. Maana wanamega kidogo, watu wanapiga kelele. Wakitulia wanamega tena. Mchezo ni huohuo mpaka mabando yatakuwa hayanunuliki tena.

Wanafanya wateja wao mazuzu, na wameungana wameunda kama cartel hivi, hakuna mtandao wa kukimbilia.

NINI KIFANYIKE?
 
Huu ni uhuni wakuu, Tigo GB moja ilikuwa 1500. Wakaleta mb 900. Juzi zikawa 750. Leo kwa 1500 unapata Mb650. Kwa hesabu
Tigo ni mali ya mzalendo wa Taifa gas, anayedai wawekezaji uchwara ni mzigo kwa Watanzania, nia abaki bila ya ushindani akifyonza na kula keki ya taifa kiulaini,Kenya walimshtukia huku anatamba yeye ndie the Don, hao wengine ni wapambe tu ingawa ndio waliomfanya afike hapo wao wamegeuka wapiga makofi.

Kwa huyu Don hata TCRA haitafanya chochote, tutawasikia akina Nepi wakiunga mkono uhuni huu, kwani wao nao ni wapiga makofi wa bwana mkubwa huyo, kuna kazi sana huko mbeleni kwani huyu bwana ni mtaka faida kiulaini na akiingia kwenye sector fulani nyie wengine inabaidi muwe watazamaji ,sote tunakumbuka tenda za migodini...
 
Tigo ni mali ya mzalendo wa Taifa gas, anayedai wawekezaji uchwara ni mzigo kwa Watanzania, nia abaki bila ya ushindani akifyonza na kula keki ya taifa kiulaini,Kenya walimshtukia huku anatamba yeye ndie the Don, hao wengine ni wapambe tu
Waziri amegeuka kuwa msemaji wa hayo makampuni.
 
Maadam watumiaji tunaendelea kuweza kununua wataendelea kupandisha. Hawana motisha ya kushusha bei wakati bado tunakamulika.

Siku watumiaji watakapopungua ya kutosha kutokana na kushindwa kuhimili bei, ndipo labda wataanza kushusha, maana faida yao itaanza kupungua.
 
Punguzini matumizi ya internet yasiyo ya lazima, Mimi natumia JF,Whatsapp,Flash Score,Sportsbet app na Twiter,

Sasa komaa na Tiktok,insta na Youtube u yonywe damu.
Watu wanafanya biashara huko Insta, na Tiktok. watu wanapata elimu huko youtube. Wengine wana gigs zao mitandaoni nk nk. matumizi ya internet ni makubwa sana.
 
Maadam watumiaji tunaendelea kuweza kununua wataendelea kupandisha. Hawana motisha ya kushusha bei wakati bado tunakamulika.

Siku watumiaji watakapopungua ya kutosha kutokana na kushindwa kuhimili bei, ndipo labda wataanza kushusha, maana faida yao itaanza kupungua.
Sisi kama watumiaji hatuna cha kufanya?
 
Kisa wanataka ufadhili waweze kuwa ma CEO wa kampuni. na CEO wa kampuni ameufyata anapoona kibarua wake anakuwa anafanya kazi kwa mtu binafsi.
Basi hii vita ya kuupata UCEO ni pana na kali sana, hadi wa hovyo na sellouts wanautaka.
 
Back
Top Bottom