Huu sasa ni wizi. Toka GB 1 kwa 1500 hadi 650 mb!

Huu sasa ni wizi. Toka GB 1 kwa 1500 hadi 650 mb!

Naachana rasmi na Instagram na app zote zinazokula data.

Nagonja kwa hamu sana siku G1 Iwe buku 7
 
Mimi nikiweka mb za wiki natumia kwa siku moja tu wakati matumizi yangu makubwa ni kuperuzi jamii forum tu.

Hili suala linatakiwa kukemewa na watu wote mana huu ni wizi wa wazi.
 
Kuna watu wanashinda Instagram na YouTube sasa huwa najiuliza wanaunga bando kiasi gani mana Mimi nikijaribu hata kusearch YouTube tu bando linaisha.
Punguzini matumizi ya internet yasiyo ya lazima, Mimi natumia JF, Whatsapp, Flash Score, Sportsbet app na Twiter,

Sasa komaa na Tiktok, insta na Youtube unyonywe damu
 
Ukiwa na mgahawa wako, kila siku ukipandisha bei watu wanajaa, ukipandisha tena wanajaa, ni lini utaacha kupandisha?

Inaonekana tunatumia zaidi social media kwa burudani na tupo tayari kuigharamia sana. Siku mauzo yakishuka ghafla utaona mambo yatakavyobadilika kwa muda huo.
 
Huu ni uhuni wakuu, Tigo GB moja ilikuwa 1500. Wakaleta mb 900. Juzi zikawa 750. Leo kwa 1500 unapata Mb650. Kwa hesabu za uwiano, hiyo mb 650 ilitakiwa kuuzwa Tsh 975. Kuna Tsh 525 nzima tumeongezewa. yaani Bei imeongezeka kwa asilimia 53 ndani ya muda mfupi tu!.

Huu ni uhuni, ni bidhaa gani zinaongezeka bei kwa kasi kiasi hicho? Sasa wakuu, nini kudeal na uhuni huu wa mitandao ya simu. Maana wanamega kidogo, watu wanapiga kelele. Wakitulia wanamega tena. Mchezo ni huohuo mpaka mabando yatakuwa hayanunuliki tena.

Wanafanya wateja wao mazuzu, na wameungana wameunda kama cartel hivi, hakuna mtandao wa kukimbilia.

NINI KIFANYIKE?
Airtel nao wameshusha unapa 985 mb kwa 2000
 
Tigo ni mali ya mzalendo wa Taifa gas, anayedai wawekezaji uchwara ni mzigo kwa Watanzania, nia abaki bila ya ushindani akifyonza na kula keki ya taifa kiulaini,Kenya walimshtukia huku anatamba yeye ndie the Don, hao wengine ni wapambe tu ingawa ndio waliomfanya afike hapo wao wamegeuka wapiga makofi.

Kwa huyu Don hata TCRA haitafanya chochote, tutawasikia akina Nepi wakiunga mkono uhuni huu, kwani wao nao ni wapiga makofi wa bwana mkubwa huyo, kuna kazi sana huko mbeleni kwani huyu bwana ni mtaka faida kiulaini na akiingia kwenye sector fulani nyie wengine inabaidi muwe watazamaji ,sote tunakumbuka tenda za migodini...
Hata voda imepanda
 
Bado tuendelee kumsimanga Baba jesca au tubaki tunaimba tutamkumbuka. Hii nchi saiv ipo mikononi mwa walamba asali wachache
 
Back
Top Bottom