pesakilakitu
JF-Expert Member
- Aug 17, 2024
- 1,618
- 2,861
Jamani Tanzania ni nchi ya amani, na pia katika upande wa michezo tunaamini katika fair play na uhuru wa kutoa maoni bila kufanyiwa ukatili.
Kuna video inasambaa kwa kasi kubwa mitandaoni ikimuonesha shabiki wa Yanga akijaribu kutoa maoni yake na kuwafariji mashabiki kua ni hali ya mchezo wa mpira wa miguu ukifungwa unakubali unajipanga.
Lakini katika hali usiyo ya kawaida walitokea wanaosemekana ni MAKOMANDOO wa Yanga na kuanza kumpiga shabiki huyo makofi na ngumi na mateke, na kijana wa watu japo alikua anakimbia kujihami lakini bado walikua wanamkimbiza huku wakiendelea kumshambulia.
Jambo hili ni baya sana na linachafua mpira wa miguu. Uongozi wa yanga ukishirikiana na mamlaka za kisalama pamoja na Bodi ya Ligi ziwachukulie hatua kali sana WAHUNI hao wanaojiita makomandoo wa yanga.