KERO Huu uchafu mtaroni hapa Sinza Africasana, wahusika hawauoni au hakuna wa kuwajibika?

KERO Huu uchafu mtaroni hapa Sinza Africasana, wahusika hawauoni au hakuna wa kuwajibika?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Salaam Wana JF

Hapa ni Sinza Africasana, mtaro wa upande wa barabara ya kuingia Mabatini police

Je, mamlaka hazioni hili? Lakini pia Wananchi tunawajibikaje kulinda mazingira yetu? Na ukizingatia tumeambiwa kuwa mvua kubwa zinakuja zikileta maafa?

1787907691577.png


​
Pia soma
~
Rais Samia: Dar es Salaam ni kuchafu, ni aibu
~ DC Mpogolo: Atakaye tupa taka Ganda la Ndizi na Pipi faini Milioni 1, Dar
 
Wabongo watu wa ajabu sana, kuzibua tu hapo mtihani, sijui kipi angalau tunaweza.
 
Mjipange raia/wakazi ya maeneo hayo mpige usafi wenyewe,akija diwani sijui Mtendaji mtoeni mbioo
Nyie jitoleeni msafishe tu

Ova
 
Maendeleo yanaanza na wewe mnataka usafi fanyeni wenyewe hao wahusika ukute hawaishi hapo na hawajali,mwisho wa siku magonjwa mnapata nyie na gharama za kujitibia ni zako serikali haitakuokoa na kila kitu wala kutatua kila lalamiko,na mvua zikianza hapo mtalia. Na huo uchafu sio ajabu nyie wenyewe ndo mnatupa mnaona sawa tu mpaka siku liwakute kama hilo uje jamii kulalamika.
 
Mjipange raia/wakazi ya maeneo hayo mpige usafi wenyewe,akija diwani sijui Mtendaji mtoeni mbioo
Nyie jitoleeni msafishe tu

Ova
Mkuu, hiyo sehemu ni ya jiji na watu wanalipa kodi. Yaani wakilogwa wakifanya hivyo basi watawala walivyo wajinga wataona huo ni wajibu wa wananchi. Ushauri mzuri ni kuwa wanatakiwa kuaandamana na kuondoa hawa watawala walishindwa kila kitu. Kodi wanachukuwa tena sana tu lakini fedha zianaishia kwenye Rolls royce za kina Abdul na Mcherengwa.
 
Back
Top Bottom