Huu ujauzito, nimeukataa rasmi

Huu ujauzito, nimeukataa rasmi

Kuna uzi uliwahi ku-trend sana humu jukwaani wa yule Mzee aliyewakataa watoto huko sijui Manyara na yule Mama akamhakikishia kuwa hatakaa awaone tena, saa hizi ndio alikuja kuanzisha uzi humu wa kuwatafuta....sijui ule uzi unaitwaje, dogo angeusoma akapata funzo
 
Angalia sana maamuzi yako mkuu.

Maelezo kujichanganya kwa wanawake ni kawaida sana. Hata yeye haelewi vizuri hayo mambo especially akiwa prime.

Kama kaka yako NAKUONYA BE VERY CAREFUL NA AAMUZI YAKO. Usione sifa saa hizi kujifanya kidume kukataa mimba, huwa kuna concequencies kibao mkuu kwenye kukataa mimba
Naxhkur mkuu , nimekuelewa vyema
 
historia ya kiumbe binadamu huanzia pale mimba inapotungwa....... alikuwa mpenzi wako si ndio......ila unadai mimba si yako???..unataka kutuaminisha mpenzi wako alikuwa ni MALAYA SIO!!!!....kama ndivyo na wewe ni MALAYA au sivyo???....mpaka umeamua kumla kavu ulijiridhisha ni wako....kataa au kubali dogo.......nakwambia kwa busara, lea mimba huyo ni mwanao.......una hofu tulia ajifungue....kimya kimya kapime DNA......kama sio wako..kapime na HIV........then mshukuru Mungu........mwambie mwenzio majibu kwa upole....songa mbele.....utabarikiwa....
 
Kwakweli vigezo ulivotumia kukataa mimba havina mashiko hata kidogo angalau ungepiga utrasound ukajua hata umri wa mimba na ufanye ulinganifu wako
Ushauri wangu lea mimba mtoto akizaliwa kapime DNA japo inaonekana mtoto ni wako
 
Kwako dear x! [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Habarini wana jamvi.natumai mu wazima kabisa.

Siku za nyuma kidogo nilileta Uzi humu kuhusu kutoelewa ujauzito alioupata mpenzi wangu .Na hii ni kutokubaliana na maelezo yake ambayo yanakinzana na ukweli kidizaini flani .

Kiukweli naona nabambikiwa bao la mwanaume mwenzangu kabisah. Sasa maamuzi niliyochukua ni kukataa rasmi kujihusisha na huo ujauzito wake japo messages zake za kunilaani zimezidi.

Ila naamini hazitonifika hapa (shingoni), sitonyoosha mikono juu, sitorudi nyuma.

Kwko dear ex

Wako mtiifu uliyetaka kum bambikia mtoto.

NB: Shida siyo hali ngumu, shida ni kulea bao la mwenzio.
Nenda kampime DNA,sio sawa kukataa damu iliyo yako.
 
Acha mawazo ya Kivulana, lea mtoto, unaweza kuwa hata Social Father mzee na mtoto atakufaa, jitie ujanja mwingi ila mwisho wake ni maumivu
 
Back
Top Bottom