Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
- Thread starter
- #221
Airtel ya mhindi,nmb serikali Ina hisa chini ya 32%,Kuna wazungu ndani ya nmb,pigeni kelele na huko
NMB, umiliki wake mkubwa ni wa Serikali na other local entities.
Cooperatieve Centrale Raiffeisen-Boerenleenbank B.A. wana 34.9%
Serikali 31.78%
NICOL Tanzania ina 6.61%
Other Private and Public entities wana 12.64%
Kwa hiyo, kwa ujumla, Serikali na taasisi zake na private entities wanamiliki zaidi ya 50%.
Suala siyo mzungu, mwarabu au mhindi, bali huyo anayesema ni mwekezaji, amewekeza nini? NMB, hisa zilinunuliwa kwa watu kutoa pesa. Mimi pia nilinunua hizo hisa. Na hiyo kamapuni ya wazungu ilitoa kiasi kikubwa cha pesa ili kuiongezea bank mtaji.
Sasa niambie, aliyepewa Ngorongori amewekeza nini pale? Alitoa pesa kiasi gani kwaajili ya kuongeza wanyama?
Aliyepewa misitu, alitoa pesa kiasi gani ili kuongeza idadi ya miti asilia?
Kwenye bandari, niambie DPW wanamiliki kiasi gani baada ya kutoa mtaji kiasi gani?