Huu upepo wanaJF wa kurudisha watoto kayumba kutoka EM wala sio maamuzi binafsi ni basi tu ukata umekuwa mkali

Huu upepo wanaJF wa kurudisha watoto kayumba kutoka EM wala sio maamuzi binafsi ni basi tu ukata umekuwa mkali

Tuulize saint kayumba tunavyoteseka, ukiingia interview room kiingereza kinabaki njee kikikusubiria hadi utoke, wakati huo ushakosa opportunity 😁
Achana na hawa watu mkuu.

Yani mtoto wangu aendee kugombania madawati kama nilivyogombania mimi wakati nina uwezo wa kumpeleka intl wewe labda ni chizi
 
Kama huna uwezo wa kumpeleka mwanao intl schools bora umpeleke kayumba tu. Na Kama huna uwezo wa kulipa ada za Oxford, Stanford,MIT etc usimpeleke mwanao intl schools, mana ukifanya hivyo ata graduate na kukuacha wewe kwenye ufukara wa kutupwa jalalani.
 
Wazazi wengi wakishapiga hesabu ya kwamba anamsomesha mtoto kwa gharama alafu mwishowe anakosa ajira na status yake inakuwa sawa na aliyesoma Kayumba ndo huchukua maamuzi ya kuwapeleka watoto wao Kayumba.

Peleka English medium ama international schools akatengeneze network na watoto wa decision makers. Ili hata kama wewe ni pangu pakavu bhasi yeye atakuwa na pa kuanzia

Hakuna raha ya kuwa na network ya watu ambao mnategemewa na ukoo kuukoa kutoka kwenye umaskini. Sadly, hiyo ndio network ya watoto wa st kayumba ukitoa wale waliosma dhule za vipaji maalum au kubwa za mijini ambapo kuna mchanganyiko
 
Back
Top Bottom