Inaonekana umepoteza plot ya haya majadiliano.
Mosi, hakuna sehemu nilikozungumzia 'connections'. Hilo umelisema wewe, na umesema hivyo kwa kuwa mfumo uliosomea ndiyo umekudumaza kuamini kuwa huwezi kufika juu bila kuwa connected!
Nanyoosha maelezo yangu kwa kukwambia kuwa, kuna baadhi ya shule ukisoma huwezi kubangaiza.
Kwanza zitakusaidia kujitambua nguvu na vipawa vyako. Pia, utasoma katika mazingira ambayo utaiva vilivyo katika kile unachokisomea. Usisahau kuwa watoto hawa husoma kozi zenye soko ktk upande wa kuajiriwa na kujiajiri. Hawachagui kozi ili wapate 100% za HESLB.
Mhitimu huyu hawezi kubangaiza kama mtoto anayefundishwa na mwalimu aliyepata div IV.
MWISHO.
Nakubali kuwa mimi ni masikini, lakini kubali wewe ni mshamba.
Kwa zama hizi za teknolojia hata mtu aliye Namabengo kule Ruvuma anaweza kuitafuta IST akaiona sawa na wewe unayepita kwa nje ukiwa unaenda kuoga Coco Beach!
Lakini huwezi kuyajua haya kwa sababu umesoma kwenye hizo shule zenu za kuungaunga.