Huu usajili wa Luis Miquisone ni ishara Simba hawajui walifanyalo, au wapigaji wapo kazini

Huu usajili wa Luis Miquisone ni ishara Simba hawajui walifanyalo, au wapigaji wapo kazini

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2010
Posts
60,050
Reaction score
104,466
Kwanza niweke wazi tu Mimi kwenye riziki ya mtu huwa sina mtimanyongo lakini kwa usajili wa Luis Miquisone unaleta mashaka makubwa sana.

Mtakumbuka Miquison aliondoka Tanzania akiwa kwenye peak lakini ushindani uliopo Al Ahaly akashindwa kuonesha uwezo wake, siamini kama ni ubaguzi maana yupo Msouth Africa pale Tau ni mchezaji tegemeo, kwahiyo in short ameshindwa kuonesha uwezo.

Sasa miaka mitatu bila Miquison kucheza soka la ushindani leo Simba wanampa mkataba wa miaka mitatu, je akicheza chini ya kiwango si itabidi Simba imlipe pesa za kuvunja mkataba?

Hapa ndio nanusa harufu ya wapiga madili kumbe huwa wanategeshea hadi kwenye kuvunja mikataba kote huko wapige pesa.

Namtakia heri kijana arudi na kiwango chake aweze kuonekana kwenye mashindano ya CAF.
 
Binafsi nimechagua kutoongelea lolote kuhusu usajili wa timu msimu huu, nasubiria muda utupe mbivu na mbichi. Ni yupi atakuwa kafanya maamuzi sahihi na kwa asilimia ngapi.

Mchezaji anaweza kufeli sehemu kutokana na mazingira mbalimbali lakini akaenda kwengine akafanya vizuri, au anaweza kufanya vizuri alipotoka ila anakohamia akafeli.

Au kote kote akaonesha kiwango kinachofanana. Tuache muda utoe hukumu, uwanjani ndio mahali pekee pa kupata majibu
 
Kwanza niweke wazi tu Mimi kwenye riziki ya mtu huwa sina mtimanyongo lakini kwa usajili wa Luis Miquison unaleta mashaka makubwa sana...
Sasa wewe pesa ya simba ulishawahi kuchangia sh ngapi? Watu wanatumia pesa yao wewe kinakuuma kitu gani?

Turudi kwenye suala la msingi la usajili wa Miquison. Sina uhakika kama ni kweli Miquison hajacheza kabisa soka la ushindani. Maana ujue alipelekwa uarabuni kwa mkopo, na siamini9 kama na huko hakuwa aqnapata namba!

Kama hakuwa anapata namba si kwamba ni lazima atakuwa ameshuka kiwango japo atakuwa hana match fittness. Hapo ni suala la mazoezi tu na na ku-activate makali yake!!

Ninaamini nkabisa kuwa kuna asilimia nyingi tu za konde boy kutesa sana kwenye ligion yetu. Mwanzoni tunaweza kulazimika kumvumilia kidogo wakati anajifua na kurudisha match fittness yake!!
 
Kwanza niweke wazi tu Mimi kwenye riziki ya mtu huwa sina mtimanyongo lakini kwa usajili wa Luis Miquisone unaleta mashaka makubwa sana.

Mtakumbuka Miquison aliondoka Tanzania akiwa kwenye peak lakini ushindani uliopo Al Ahaly akashindwa kuonesha uwezo wake....
sidhani kama usemayo ni kweli

Sent from my CPH2371 using JamiiForums mobile app
 
Kaka kwani Makambo na yule wa nyu kesto wako wapi? Sajiri nyingi ni kamari
Lakini Kamari ya kumpa mkataba wa miaka mitatu kuna kilichojificha hapo ambacho kwa jicho la kawaida huwezi kukiona.

Yanga kumpa mkataba wa mwaka mmoja Mkude si wajinga, wanapima upepo wake kwanza, upepo usipokuwa sawa amalize mkataba wa mwaka mmoja na Thank you yake, ila a kuonesha kiwango ataongezewa mkataba mapema tu kabla ya huu kuisha kuliko kujifunza kabla hujaona huduma yake.
 
Lakini Kamari ya kumpa mkataba wa miaka mitatu kuna kilichojificha hapo ambacho kwa jicho la kawaida huwezi kukiona...
Kaka hivi unajua josee alisajiliwa kwa sh ngapi na Al ahly?

Na mshahara wake ulikuwa kiasi gani?

Je usajili uliwalipa al ahly?
 
Kaka hivi unajua josee alisajiliwa kwa sh ngapi na Al ahly? Na mshahara wake ulikuwa kiasi gani? Je usajili uliwalipa al ahly?
Unaongelea Miquison au Josee yupi? Kama ni Miquison Al Ahaly wenyewe walimuona Simba na Simba na Al Ahaly zilikutana klabu bingwa, kwahiyo Al Ahaly walinunuwa bidhaa wanayoijuwa vizuri tu si Kwa kuingizwa mkenge na scout.
 
Back
Top Bottom