Sawa mkuu,,
Ila nilichojifunza ktk sakata zima la ugomvi wa baba diamond na diamond,,ni ufukara wa baba diamond alionao
Hivyo basi tunapaswa kutafuta pesa kwa wingi,,
kwani hakuna baba Tajiri aliyekataliwa na mwanae..
hata akatae mimba,,bado atakumbatiwa kwa mapenzi makubwa na mwanae.
Hivi Diamond angekuwa fukara huyo mzee ange mtafuta.
Baba yake Ommy kaonekana baada ya Ommy kuwa vizuri kifedha.
Baba Mwana Fa nae hivyo,je hao kama wangekuwa mafukara wangejitokeza?
Baba Diamond hakuwa fukara bali ujinga wake mwenyewe na ndio maana alivyo mwacha mama diamond akaenda kuzaa na mwanamke mwengine,sasa huwezi kusema huyu alikuwa masikini bali ujinga wake mwenyewe.
Siku zote mtoto humjali mzazi wake haijalishi ana hali gani,hata ukiwa na mia hakikisha unakula na mwanao,kwani hicho hicho kidogo kinaacha alama kubwa ya upendo na ukumbusho kwa watoto na mke wako kwani wanaona.Yaani hakikisha uwe na hali nzuri au ngumu zote unapitia pamoja na watoto wako,NAKUHAKIKISHIA UKIFANYA HIVYO WATOTO ZAKO HAWATO KUACHA KAMWE.
Cristian Ronaldo mpaka kesho anamkumbuka baba yake,pamoja walikuwa na ufukara wa kutupa lkn mzee wao hajawaacha na haja ikimbia familia.
Daniel Alves yule kapitia magumu pamoja ya wazazi wake,baba yake hakuwaacha familia yake pamoja na ufukara wake hajawahi kuwaacha watoto wake,Dan alikuwa anatembea km kibao kwenda kucheza mpira,baba yake alimsapoti kwa kile alicho jaliwa.Leo hii wanakula matunda ya mtoto wao.
Timiza wajibu wako mtoto wako hatokuacha uzeeni au unapo pitia magumu kiuchumi.