Huu uzikaji wa white people uko poa sana watu 10 wanamaliza msiba kabisa.

hio culture iko poa sana
 
Nadhani na nyie kufika hapo malaloni ni kwa sababu ya taratibu za jamii mlipokulia...
Exactly, vinginevyo tusingeenda.

Kuna sehemu nyingine ukienda makaburini kuzika kama si mtu wa familia watu wanakushangaa, wanajiuliza huyu anatafuta nini? Kuna kitu anatafuta.

Mambo yote yanaishia Funeral Home.

Hawaamini kuwa unaweza kwenda kumzika mtu kwa urafiki tu.
 
Kuna mzungu flani ilibidi aulize baada ya kuona kundi kubwa la watu wanakwenda makaburini, watu walikuwa wengi, kama ujuavyo, jamaa akauliza marehemu yaelekea alikuwa mtu maarufu sana, akaambiwa hapana ni mtu wa kawaida tu, basi alishangaa sana.
 
Mpaka tule wali mzee, matanga wiki nzima, tunapiga chai na mandazi kupitia rambirambi. Kiafrika msiba ni mchongo, mida ya misosi unajisogexa msibani, ukipiga msosi unasepa. 😁
Waafrika tunaishi dunia yetu kivyetu, unaweza kuta watu wanalalamika msosi kuwa mdogo msibani au wanausifia sana msiba kwa sababu ya msosi na pombe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…