Huu uzikaji wa white people uko poa sana watu 10 wanamaliza msiba kabisa.

Huu uzikaji wa white people uko poa sana watu 10 wanamaliza msiba kabisa.

Huku Africa kuna wale wakuangalia nani hayupo msibani tuje na sisi tumsusie kwenye msiba wake.
Hao wengi sana. Hii habari imenikumbusha mbali sana.

Nishaenda kuzika mzee mmoja mkazi wa New York City. Yule mzee alikuwa landlord wetu miaka hiyo ya nyuma ya 1990s wakati nafika New York City. Alikuwa askari wa zamani, veteran wa US Army wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Yule mzee alikuwa anaishi mwenyewe chini, na wapangaji tulikuwa tunaishi juu. Alikuwa mtu poa sana kwetu.

Sasa siku moja winter ikanyesha snow, akawa anasafisha mbele ya nyumba yake. New York na sehemu nyingi Marekani kuna sheria kali sana za kutaka wenye nyumba wasafishe snow mbele ya nyumba barabarani (sidewalk) ili watu wanaopita njia wasianguke kwa kuteleza kwenye snow, ukichelewa kusafisha halafu mtu akaanguka unaweza kupewa kesi kubwa sana ya kulipa mamilioni ya pesa.

Kwa sababu hii, yule mzee alifanya juhudi kusafisha snow. Unajua mtu akishakuwa askari tena hata akizeeka anakuwa anajiona yeye bado anaweza kazi ngumu. Basi, kumbe katika kusafisha ile snow, moyo wake ukalemewa akapata matatizo mpaka akafariki.

Wakati anafariki mimi nilikuwa nishahama hapo kwake nimenunua nyumba nimehamia kwangu, ila kuna jirani yangu mmoja tulikuwa tunakaa naye akanipigia simu kunipa habari landlord wetu wa zamani amefariki.

Nikasema huyu mzee tulikaa naye poa sana. Alikuwa anapenda kukaa nje akiniona narudi kutoka kazini ananisifia sana ninavyopendeza nikivaa suti zangu natoka Wall St. kazini. Na mimi mara nyingine nikikaa naye barazani akinipa stories za ujana wake, alivyopigana vita, maisha, na kadhalika. Kwa hivyo nikaenda kumzika.

Marekani kuna utamaduni wa watu kukutana Funeral Home kuangalia mwili kama last respects, halafu watu wengi wanatimka hapo, wachache wanaenda makaburini kuzika. Ndiyo maana unaweza kuona picha makaburini watu ni wachache, kwa sababu wao wanaona kitu muhimu ni kwenda kanisani au kwenye funeral home, huko makaburini mtu anaweza kuzikwa na watu wachache tu.

Na kweli, ndivyo ilivyotokea kwa huyu mzee. Walikuja familia yake, mama mtoto wake na huyo mtoto binti, ambao alikuwa anaonana nao mara chache sana. Lakini waliishia kwenye funeral home.

Yule mzee watu tulioenda makaburini kumzika ni wawili tu, ambao walikuwa ni mimi na yule mama wa ki Jamaica jirani yangu wa zamani aliyenipigia simu kunijulisha msiba.

Hata mama mtoto wake na binti yake yule mzee hawakwenda makaburini kumzika.

Bahati nzuri mifumo ya huku wafanyakazi wa makaburini wana vifaa vyote vya kutayarisha kaburi na kumzika mtu, kulikuwa na matrekta maalum ya kazi hii, haikuchukua muda.

Ila nilijisikia vibaya sana mtu kazikwa na watu wawili tu, tena wala si ndugu zake ni watu alioishi nao tu kama wapangaji wake.

Hii story imenikunbusha sana maziko hayo, nikaona hawa wa kwenye picha mnasema wachache? Sisi tulimzika landlord wetu tukiwa watu wawili tu.
 
Back
Top Bottom