Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,973
- 6,750
Well mimi sidhani kama watu wanazuiwa kutoa maoni.Kinachozuia ni matumizi mabaya ya uhuru wa kutoa maoni..Tuelewa maoni sio maelekezo wala sio amri.Unapotoa maoni yako kwa staha haimaanishi kwamba uko sahihi.Kwa mfano kwenye uzi huu mimi nilichotolea maoni ni matumizi ya lugha ya matusi tu kwenye kadamnasi.Inawezekana siko sahihi ila nimetoa maoni na sijazuiwa.Ila unafikiri nikianza kumtukana huyu aliyetukana nitakuwa ninatumia uhuru wangu vizuri?Au mimi na wewe tunavyopeana majibizano hapa mara ghafla nikaanza kukutukana nitakuwa natumia uhuru wangu wa maoni vizuri?Uhuru unapokuwa hauna kikomo unakuwa tena sio uhuru bali ni kero.Tukubali kama jamii tumefika katika hali hii kwa sababu tumejisahau na tunasahau kabisa kwamba Sio wakati wote tuko sahihi.Mkuu unapozuia watu uhuru wao wa kutoa maoni yao mambo kama hayo si ajabu kutokea, sio kwamba mimi naona sawa hayo matusi hasa kwa mzee kama yule bali naangali kipi chanzo kilichotufikisha hapa kama taifa? Maana si matusi tu bali tumefikia hadi kufurahia vifo vya watu.
Lazima tuwe na maadili na tusiogope kusema haya sio maadili yetu hata kama tunaonekana kukosea au hata kama dhamiri zetu zinatuumbua