Huu wizi kupitia Tigopesa, naomba Tigopesa mnisaidie majibu hapa

No SQL

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2014
Posts
7,063
Reaction score
12,563
Kuna watu wawili wamekuja kutoa pesa kwangu 'wakala' .. wa kwanza katoa 450,000 na wa pili katoa 500,000 Wote hawa namba yao ni moja 252659 234042 lakini majina ni tofauti. Mmoja jina lilikuwa 'Daniel Michael' na wa pili jina lilikuwa ' Jonh Joseph'.

Wakati wa kutoa waliomba namba ya wakala na meseji kwangu ilikuja kawaida kama miamala mingine... na pia salio liliongezeka kama ilivyotakiwa.

Baada ya muda, kuangalia salio naona pungufu ndipo nikapiga simu tigo na kuambiwa kwamba hakuna miamala hiyo iliyofanyika.. sasa angalieni hizi picha na muweze kutoa majibu.

 
Mmmh pole sana. Uzuri ushahidi wa sms unao. Ngoja tusubiri wataalamu waje.

Umejaribu kumpigia huyo aliyetoa pesa? Hizo namba zinaanzwa na 252???
 
mbona namba iliyoleta text zote inaonekana ni TIGOPESA?
 
Jibu kama simu zako zilishikwa na hao matapeli, leo au days before...

Kama walizishika tafuta mtu anaitwa TIGOPESA kwa phonebook yako ukimkuta, liaaaaaa... Kisha endelea na bness, chukulia kuwa umelipa ada ya mafunzo as hutaibiwa tena na hakuna mtu atagusa yo phone again!
 
Ila nadhani Kama alimpatia mteja simu Kuna mistake na kuna kitu wamefanya jamaa
Mkuu kuna mchezo wamefanya wamemtumia text inayoonekana vile vile kama ya TIGOPESA na mpka no ni ya tigopesa.

Hapo tigo hawana tatizo washampiga maskini maana hakuwa makini kuangalia hiyo namba, inaanziwa na "252" code za tanzania ni 255
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…