Hapa niseme neno, kuna baadhi ya watoa huduma za fedha kuepuka usumbufu wa kuingiza namba isiyosahihi, huamua kumpa mteja simu na kumwambia ingiza namba. Yule mteja kama si mwema, anacancel kwanza kisha anasave kwenye simu yako namba ambayo atakuja kukupiga nayo mwenzake hapo baadae au hata kesho yake, namba anaisave kwa herufi kubwa TIGOPESA au MPESA. Kisha anakwambia hebu rudia kuniwekea ile sehemu ya kuweka namba, anakupa simu, unabofya tena, unampa simu, anaingiza namba sahihi, unamrushia hiyo buku mbili yake, anasepa.
Kesho yake, anakuja mtu na mazungumzo yenu yanakuwa kama hivii
Mteja: niingizie milioni mbili. (Anatoa burungutu lamilioni mbili kweli)
Wakala: salio halitoshi bosi
Mteja: dah, una kiasi gani?
Wakala: ngoja nicheki
Mteja:..............................
Wakala: laki mbili na nusu
Mteja: Anahesabu laki mbili na nusu, anampatia wakala."Niingizie hiyo hiyo"
Wakala: Anapokea hela na kukamilisha muamala.
Mteja anatembea zake huku anajua kwenye float uko kapu.
Baada ya dk 3 anakuja mteja wa kutoa
Mteja: nataka nitoe laki tano
Wakala: Toa
Mteja: Anabonyeza bonyeza, kisha anakufowadia messeji ambayo wakala hupokea pindi mteja atoapo pesa, namba ya huyu mteja anaekutumia meseji ilishaseviwa kwako kwa jina la TIGOPESA. So meseji ikiingiza itaonekana kweli imetoka TIGOPESA, lakini fake.
Wakala: Unatoa laki tano keshi.
Baada ya dk 3 tena anakuja mteja wa kutoa
Mteja: nataka nitoe laki nne
Wakala: Toa
Mteja: Anabonyeza bonyeza, kisha anakufowadia messeji ambayo wakala hupokea pindi mteja atoapo pesa, namba ya huyu mteja anaekutumia meseji ilishaseviwa kwako kwa jina la MPESA. So meseji ikiingiza itaonekana kweli imetoka MPESA, lakini fake.
Wakala: Unatoa laki nne keshi.
Ukiangalia salio halisi, umeliwaaaaaaaa.