Huu wizi kupitia Tigopesa, naomba Tigopesa mnisaidie majibu hapa

Wizi huo alishawahi kukamatwa mwizi na video ilisambaa sijajua ilikuwa wapi.

Pale unapompa aweke namba ya siri yeye hufanya fasta kuisave namba yake kwa jina la TIGOPESA. Kwenye hio meseji, itizame hio contact sasa.
 
Ndo maana yake...!!! Nakumbuka mitandaoni siku za nyuma kulisambazwa clip fulani ya mwizi mtaalamu wa kompyuta ngazi ya diploma; alikamatwa na akawa anahojiwa na polisi kwa kichapo kikali akaelezea namna wanavyoiba akasema hivyo hivyo wanavyoeleza watu humu...

kwamba anaenda kwa wakala anaomba huduma halafu itafika kipindi ataomba simu ya wakala (ili aweke namba ya siri nadhani) na kwa haraka sana (si zaidi ya sekunde 30) atafanya matendo mawili

moja ni kuingiza contact mpya kwenye simu ya wakala kwa kusevu jina la kampuni mfano tigopesa au m-pesa au airtel money n.k na pili ni kuangalia sms ya muamala wa mwisho

Baada ya hapo ndo anatafuta sms yoyote aliyonayo ya kuhusu miamala kwenye mtandao husika kisha anaiedit panapohitajika halafu akija kwako anajifanya ametoa pesa kumbe anakuforwadia ile sms

Nawashauri mawakala wawe na utaratibu wa kukagua mara kwa mara phonebook zao pia wasizihusishe simu/ laini za kazi yao ya uwakala na mambo ya mawasiliano (laini ya kazi iwe ya kazi tu) kwani ndicho chanzo cha yote hayo

Pia mitandao ingefanya utaratibu wa kutofautisha (kama walivyotofautisha kwenye gharama za usajili) laini za kiuwakala na za mawasiliano kama ingewezekana laini ya wakala mtu asiweze kuitumia sms wala kuipigia
 


Hii ndo njia sahihi. Nadhan over time watalifanyia kazi.
 
Bongo ni nchi iliyojaa wazembe na wengi tumezoea kufanya vitu kwa mazoea ya kuigana. Nina uhakika wakala yeyote akiwa makini ni vigumu kutapeliwa. Tubadilike tumezidi kutokuwa makini.

Pia hizi kampuni za simu zinabeba lawama. Kwa nini hazifanyi jitihada yoyote kuondoa loopholes za utapeli kama huu? Ni siku nyingi watu wanalia kwa tatizo hili hili lakini wao hawajali kabisa.
 
Nilishaibiwa laki sita na ni tg pesa kwa kweli wabadilike la sivyo tunaacha kufanya kazi na miamala yao. Wizi kwa mpesa ni kama hakuna
 
bora umemalizia vzr,ila ungeishia kuwalaumu pekee mawakala ningekushangaa,. Umakini unakuwepo ila kuna siku tuu utaingia kwny 18 zao cheki mfano hzo msg kama una wateja wengi unasahau kuangalia salio kwa kubonyeza namba unaishia kuangalia salio la kwny msg
 
Ukiwa makini hutasau hata kama una wateja wengi. Ikiwezekana andika hatua zote kwenye karatasi uiweke mbele yako. Haya malalamiko ya kuibiwa ni mengi sana na inatokea mara mara. Tukubali tu wabongo hatuko makini kwa vitu tufanyavyo.
 
Matapeli wa aina hiyo kwanza huanza kutoa pesa au kutuma kihalali halafu hutaka kuona message ya muamala uliofanyika ukimpa tu simu kwanza anaangalia Salio lililobaki halafu hu-save jina lake kwenye simu hiyo ya wakala hujisave mfano TIGOPESA, halafu hujidai anataka kutoa pesa ukimruhusu anakutumia message aliyoi-edit itakuja kwa jina la TIGOPESA.
 
Alafu voda huu ujinga siusikii kama tigo na airtel
 
Bora umemchana kubwa jinga huyo, anazeeka na upumbavu wake, kuandika tu hajui hilo pididy
Mbona wewe huwa unatuchosha na thread zako ambazo hazina maana,bwege we!
 
Hizo msg wanazituma wao kwa namba yao ya magumashi iliyoseviwa kwenye phonebook yako kwa jina la TIGOPESA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…