Huu wizi kupitia Tigopesa, naomba Tigopesa mnisaidie majibu hapa

Inamaana 450,000/= na 500,000/= zote sms hewa(editing sms).
 
Wale mliofanya miamala ya tigo pesa inamaana hizo kumbukumbu namba n za leo tarehe 11/06/2020?????
 
Majina mawili ya mwanzo tofauti lakini la mwisho limefanana, 'Mrejaa',

Mmh
 
Pole Sana Mkuu Mimi walinipiga wiki 2 zilizopita na majina ni hayo hayo, hawa jamaa nadhani Wana utaalamu wa kujua salio lako, Kwa sababu wakifika huwa wanachukua muda mrefu kutoa Pessa na akiwa anatoa unatakiwa uwe makini Sana, anachokifanya akishajua salio lako la Tigo anajumlisha na kiasi cha Pesa ambacho anqchodai anakitoa halafu anituma kama MSG ya kawaida na ikija kwako inakuja kama MSG YA kufanya muamala ukishampa hela basi ndiyo hapo anakupiga hela, kulikwepa hill wakina hawa wenye miamala mikubwa akishatoa angalia taarifa ya Miamala hawa jamaa wanaumiza Sana, Pole Sana Mimi wameniliza hao
 
Sijui anaona noma gani kulijibu hili swali
Nimeshajibu pale..simu hawajashika na hata hivyo wasingeweza kupewa simu sababu kulikuwa na wateja wanne wote wanatoa tigopesa...hao wawili walitoa fasta na wakati wengine wamemaliza kutoa ndio likaja salio halisi...kushtuka kumekucha
 
Anyway sasa hivi nimempa utaratibu anaekaa ofisini.. mtu akitoa pesa ndefu achek kwanza salio ndio apewe..
 
Anyway sasa hivi nimempa utaratibu anaekaa ofisini.. mtu akitoa pesa ndefu achek kwanza salio ndio apewe..

Ila wewe jamaa watu wanakwambia uangalie phonebook yako uone kama kuna jina limeseviwa TIGOPESA wewe unakomaa kubisha na kuuliza maswali yako ya kizwazwa ati salio wamejuaje.

Ndo maana umeibiwa kifala sababu nimeshakuona kama una akili za kichukumbe kabisa.

Shenzi taipu.
 
Daaa pole Sana mkuu ...Kuna siku nikiwa town nakula misele nyuma yangu kulikuwa na washkaji kama Watatu hivi.
Sasa kwasabu sehemu niliyokuwa napita ni vichochoroni nikawa makini kugeuka nyuma baada ya hatua kama tano hivi kwasabubu wale jamaa walikuwa wanapiga story baasi nikawa nawasikiliza bila wao kujua maana nikazuga naongea na simu.

Hii yote nibaada ya kuckia wanapiga story za miamala ya magumashi ....aisee nilichoka maana jamaa akawa anamweleza mwenzie kuwa Jana amefanikiwa kutoa sehemu milioni moja. Sasa wakiwa wanaendlea na story zao wakaanza kukumbushana mission zao zilizogoma ,mmja anasema Songea aliacha laki nne.

Mwingine anasema Mtwara alimanusura akamatwe aliacha laki nane baada ya wakala kumwambia nioneshe msg yako yakuwa umetoa ela kwangu na kwa jinsi nilivyowaelewa wale jamaa inaonekana wanaprogram flani au wanashirikiana na baadhi ya watu wa system za simu kufanya uhalifu huo.

wale jamaa inaonesha niwenyeji wa Dar nilihisi hvyo kutkana na rafudhi yao .,.na pia baada tu ya kukamata main road walikodi bajaji afu sehem wanayomweleza bajaji awapeleke ni umbali kama wa mita mia tu....chamsingi nilichogundua mtu akitoa hela chunguza vizuri muamala ule na akuonyeshe na muamala kwake pia
 
Hilo jina la tigo pesa wamesevu kwenye cm yako,kama sio Leo basi walishapita tena ofisini kwako. Ni kosa kubwa wakala kumpa mteja cm eti aandike # zake.

Wengi huwa wanatumia mbinu ya kuongea na cm akishakuambia Niwekee pesa, Ukifika pale kwenye kuingiza # atakunyooshea mkono ili umpe aandike Kwasababu anaongea kwa simu hivyo hawezi kukutajia.Ukimpa Ndio hapo anaposevu # zake kwa jina la mpesa,tigopesa nk
Kisha atakurudishia uendelee na muamala kama kawaida.

Hapo ataamua kama wakurudie siku hiyo au kesho yake kuja kukupiga hela.
 
Hapa ndio Tigo?nenda polisi au ofisi ya Tigo huku ulikokimbilia ni sawa na unampigia gitaa mbuzi.
 
Mkuu Nakuhakikishia hakuna fault ya hivo kwenye mitandao ya cm kwamba wanaweza kucheza na system bila wewe mwenyewe kuzembea.
Woote hao wanafanya mchezo wa kusevu # zao kwenye cm ya wakala. Ni uzembe wa wakala kumpa mteja cm yake Si kumuonesha mteja sms ya muamala kwenye cm ya wakala
 
Kweli huyu poyoyo hataki kujibu Hilo swali. Kwanini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iyo code pia ni swali jingine mkuu
 
Hoo staili alipopigwa ni pale wakala unaruhusu mteja kushika simu yako ili kuandka no zake za kumuwekea hela..anajisave tigo pesaa au mpesa ...Apo kipigo ndo hufuata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…