kajekudya
JF-Expert Member
- Sep 24, 2015
- 2,466
- 4,916
Ais the same to me. Nimeshalalamika sana naambiwa nilijiunga, lakini sijawahi, kila nikiweka vocha wanapita nayo, so siku hizi natumia tu halopea kununua mda wa maongezi
Hawa jamaa nawaita wezi kwa sababu wameniunga na huduma ambayo Mimi siipendi Wala sio kwa matakwa yangu
Huduma hii mwanzo walikuwa Kila siku wanakata sh 100 kwenye Kila vocha ambayo naingiza
Wiki iliyopita nikaamua kuwapigia
Mhudumu wa kwanza : akadai Kuna huduma ya halosoka nilijiunga hivyo hivyo nikitaka kujiondoa nitume neno ONDOA kwenda namba 15603
Nikajaribu kutuma hio text mara nyingi bila mafanikio nikajua labda wanataka vocha nikajaribu kuunga vocha bila kifurushi napo wapi
Nikaamua kupiga Tena , huyu mhudumu wa pili akasema nitume neno OFF kwenda namba 15603
Nikajaribu Tena na tena lakini wapi
Nikapiga Tena huyu mhudumu wa tatu akasema nizime simu then niwashe na Kisha nitume Tena neno OFF kwenda namba 15603 na kweli nikazima na kuwasha lakini hali ikawa vile vile
Nikapiga Tena huyu mhudumu mwingine akasema analiwasilisha kwa kitengo husika ndani ya masaa 24 watakuwa wameondoa . Lakini yalivopita Hali ikawa vile vile na hela nikaendelea kukatwa. Nikaamua kukubaliana na hali yao so nikitaka kifurushi Cha 2000 basi nanunua vocha 2500 Ili wakate na 100 yao
Lakini Juzi nimetulia zangu simu Ipo mfukoni nikaona mlio wa text kutoa simu na kufungua nakutana na message kuwa nimefanikiwa kujiunga na huduma Fulani hivyo nikitaka kujiondoa nitume neno ONDOA kwenda namba 15603 na ada ya huduma ni sh 100 Kila siku
Na Kila nilijaribu kutuma neno ONDOA kwenda hio namba 15603 message haziendi na kwa saivi Kila nikiweka vocha nakatwa sh 200
Nimejaribu kuwapigia customer care majibu yao ni kama wahudumu wa kwanza wale na hakuna ninachosaidiwa
View attachment 2505673
Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app