Kufunguliwa kwako kuwa huru kweli kweli kunatokana na kutokupata maarifa sahihi ya ufunuo wa Kristo.
Mambo gani unapaswa ujaue pasipo shaka?
1. Kujua kwamba Mungu hatumii mambo maovu kuonyesha uweza/nguvu/utukufu wake.
2. Mateso na maonevu ya shetani kwa watu sio jambo la fahari kwa mtumishi wa Mungu kujipatia sifa/umaarufu bali kudhihirisha pendo la Mungu na huruma yake kwa watu wake.
3. Kujua kwamba mamlaka katika jina la Yesu hairejei katika herufi Y-E-S-U bali iko katika kuongelea utambulisho wa Yesu, nafasi yake, na mamlaka yake kama matokeo ya yote aliyofanya katika kufa, kuzikwa na kufufuka kwake vyote ikiwa ni kwa ajili yako mwamini.
4. Kujua kwamba katika ufufuo huo wewe mwamini una utambulisho mmoja na Kristo, alicho nacho Kristo ndicho ulichonacho mwamini. Nafasi ya Kristo ni nafasi ya mwamini, mamlaka ya Kristo ni mamlaka ya mwamini.
5. Kujua kwamba wewe mwamini umeketishwa mkono wa kuume wa Baba yaani (sio kama kuna kiti kulia na kushoto kwa Mungu bali) ni nafasi au sehemu ya mamlaka. Ni juu sana kupita falme na mamlaka. (Efeso 1: 19-23 na 2:6)
6. Kujua kwamba wewe mwamini unapaswa kujenga ujasiri ktk hilo jina. Ujasiri huo utakuja tu kwa maarifa. Pasipo maarifa utatembea katika mashaka na hofu, utatembea ukiwa dhaifu katika utendaji kwa hilo jina.
Bila shaka ungependa kupata maarifa zaidi. Si ndio?
Mwalimu wangu Mch Felician Makarios Phos amefundisha somo hili la "Jina la Yesu" na kuweka masomo ya audio sehemu ya 1hadi ya 4 katika Telegram channel ya "KainosMedia" bure kabisa.