Huwa mnaishi vipi Kwa kutegemea mishahara?

Huwa mnaishi vipi Kwa kutegemea mishahara?

Hapa sizungumzii wale watu wenye kazi kubwa walau kuanzia million 2 kwenda juu, ambao najua hawa ni wachache mno

Hapa nazungumzia hizi kazi za kati kama manesi, polisi, walimu, bank teller nk, ambazo hizi ndo kazi za watu wengi

Yaani unakaa mwezi mzima unangoja 500k na kila siku upo kazini na sare zako au na kalamu mfuko wa shati,
Hizi ni akili au matope

Wengi wanataka job security yaani ule uhakika kuwa Utaipata hiyo pesa

Harakati za kufanya mjini na vijijini ni nyingi mno na kupata zaidi ya hicho kiduchu unachopata

Acheni huo utumwa wa hiari acheni kazi mje mtaani tupambane hadi serikali iamue kuongeza maslahi ya kuwapa heshima watumishi wa umma

Wabunge, mawaziri wao wanalipana mamilion Kwa vikao vya kupiga makofi meza, nyie mpo mnalipwa pesa nyanya

Tuambizane ukweli huwezi ukalipwa hako ka pesa
Ukasomesha watoto shule Bora
Ukatibiwa hospital nzuri
Huwezi kufanya utalii hata Mikumi
Huwezi kumiliki hata ICT
Utaishi Kwa mikopo na msongo wa mawazo
Mkuu kwani wamezuiliwa kufanya mishe zingine huku wanapokea hako ka mshahara? Wafanyakazi wa serikali hata wakipokea hicho kidogo wana madeal mengi mno ndiyo maana wameridhika! Fursa za kufanya mambo yao binafsi ni kubwa mno na hakuna ufuatiliaji! Mimi nilikuwa huko idara ya mifugo, muda mwingi nilikuwa nafanya yangu tu kazini unajionyesha angalau mara 5 kwa mwezi! Tena ukiwa vijijini ndiyo kabisaaaa!
 
Back
Top Bottom