Huwa mnakumbuka nini enyi wanaume

wanakera sana[emoji41] [emoji41]
Mnoo.....

Same shit happened to me.


Namwangaliaga tu anavyorukaruka kama maharage kwenye sufuria.

Ameishia kumlaumu mama ake kuwa ndiye alimponza baada ya maisha kumuendea kombo. Anadai angenioa mimi angekuwa mbali kimaisha.

Sisahau siku ananiambia kuwa ameamua kumuoa mwanamke aliyezaa naye pumbaffff
 
yaan usirudi nyuma kabisa kimawazo mwache aende maumivu yamekwisha ndo anarudi hajui kama kachelewa
 
yaan usirudi nyuma kabisa kimawazo mwache aende maumivu yamekwisha ndo anarudi hajui kama kachelewa
Sinaga hata time naye,analalamika kuwa mama yake ndiye alimwambia kuwa mwanamke aliyezaa naye ndiye waif matirio, kipindi hicho mie bado nasoma,mama ake akamwambia huyo msomi atakusumbua. So leo anajuta alioa mwanamke hajui maana ya maisha na tayari walisha achana.

Amebaki analalamika kwa ndugu zangu kuwa mimi ndo nilikuwa perfect choice kwake.

Mimi niko na familia sasa hivi amebaki kuona gere.
 
safi sana amfate mama ake amuonyeshe mke mwengine
 
Mbn hata nyie wanawake huwa mnarudi sana mfano mm mwanamke wangu aliniacha eti kisa tuu nimenda jeshini bada ya miaka mitatu kuwa officer wa Jeshi now ananisumbua virungu kibao mara oooh cjui cna ajira cjui chiko nikope laki 3 nitakurudishia cjui Chiko nataka nisome law school unanishaurije cjui ww ndo mwanaume wa maisha yangu wakati mwanzo alisema siwezi date na mwanajeshi mana wengi wenu nyny wanajeshi amko romantic saiz nikamuacha iyo ilikuwa 2014, saizi kaona mpunga upo ndo anajileta mana 2014 nilikuwa choka mbaya balaa leo msumbufu balaaa co mnatusema cc tu wanaume nyie jee??? tena nyny ndo wasumbufu balaaaa mesaji kuanzia asbh mpaka usiku mda wa kulala hadi kuamshwa unamshwa asbh mtu unamshwa..mnaforce kuonana balaaa wakati nyuma mtu alikuwa kuonana na mimi hataki mpaka nimuanze tena tukionana atumalizi 1hr mtu uyo kasepa na wai home dah ila maisha aya.
 
safi sana amfate mama ake amuonyeshe mke mwengine
Hahahahahaaaaaa



Kwa kweli.


Shost huyu kaka alikuwa na niya ya dhati,aliwekeza sana kwangu,alikuwa anampenda sana mama yangu,na tuna nasaba ya mbali pia, mama yangu alivaa sana vitenge na kijana alitangaza kabisa uchumba. Kila mtu pale kwetu alijua kuwa flani mchumba ake ni flani. Akaweka miadi ya kunivisha pete. Akalifikisha rasmi kwa wazazi wake. Hapo ndo meza ikageuka kichwa chini miguu juu. Kuna mwanamke alizaa naye akiwa masomoni mkoa flani, ndo mama ake akamwambia kuwa huyo mwanamke aliyemzalisha huko akiskia kuwa anaoa mwanamke mwingine atamuua kwa uchawi.

Wakamtolea na mifano mingi jamaa akaogopa. Nikaanza kuskia hizo fununu. Mwisho wa siku akanitoa outing akiwa na dada ake na ndugu ake mmoja....

Baada ya kutia story sana huku nikiwa na bonge la tabasamu ndo akaanza kunipa stori za mifano ambayo sikuielewa,ikabidi aniambie ukweli,tabasamu likageuka kuwa kilio....

Nilihisi nakufa siku ile,yani mpaka nikawa naona maruwe ruwe. Nilipata msongo mpaka nikawa najihisi kama nitakuwa kichaa..muda ni tiba,baadae nilizoea ile hali,nika move on na maisha yakaendelea. Sikujiingiza tena kwenye mahusiano mpaka alipokuja baba chanja niliyenaye kwenye ndoa. Harusi yangu mama ake na baba ake pia walihudhuria.

Kwa sasa ananiomba niwe hata nampigia simu kumsalimia na namba yake nilishaitupa na kum block kitambo sana.
 
Aiseeeh.
 
hongera mpenz
 
Hapo ukihadaika kidogo tu anakuharibia kila kitu.
Hapana Daby ...

Chaaaa......mie huyo...!?

Aisee yule jamaa hapana. Baada ya kugonga mwamba huko aliko imebidi sasa lawama ambebeshe mama yake.

Kwa bahati nzuri mama yake alikuwa anamnusuru na kulogwa kumbe ndo kamloga kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…