Unajua kuitwa soka la burudani kunatokana na theory ya wengi wape ila wengi uona kuwa ndiyo burudani haimaanishi kuwa wachache wasioipenda hiyo unayoiita burudani itakuwa burudani na kwao.Lakini haijawahi kutokea soka la Mourinho likaitwa Burudani, hivyo hilo soka unalopenda wewe sio soka la Burudani yaani Entertaining Football au Sex Football, sasa ukiamua mwenyewe kuliita hilo soka lako kuwa Soka la Burudani hicho kitakuwa kiburi chako tu[emoji23][emoji23][emoji23]
Hii theory ya wengi wape imenikumbusha swali la kama tungezaliwa wengi wetu ni zeruzeru, wale wasio zeruzeru tungewaita walemavu wa ngozi?
Soka la burudani kwangu mm ukiachana na wengi wape ni lile lenye hamsha hamsha golini kwa mpinzani na si pasi fupi fupi katikati ya uwanja. Kuna chenga na mbwembwe ambazo pia ni burudani mfano Ronaldinho alichokuwa anafanya, ila inapendeza sana hizo mbwembwe zikisababisha goli au hamsha hamsha golini kwa haraka.