Huwa Sipendi kuangalia mechi za Simba naibia naangalia Mpira ukiisha naanza Umia Rohoni

Unajua kuitwa soka la burudani kunatokana na theory ya wengi wape ila wengi uona kuwa ndiyo burudani haimaanishi kuwa wachache wasioipenda hiyo unayoiita burudani itakuwa burudani na kwao.

Hii theory ya wengi wape imenikumbusha swali la kama tungezaliwa wengi wetu ni zeruzeru, wale wasio zeruzeru tungewaita walemavu wa ngozi?

Soka la burudani kwangu mm ukiachana na wengi wape ni lile lenye hamsha hamsha golini kwa mpinzani na si pasi fupi fupi katikati ya uwanja. Kuna chenga na mbwembwe ambazo pia ni burudani mfano Ronaldinho alichokuwa anafanya, ila inapendeza sana hizo mbwembwe zikisababisha goli au hamsha hamsha golini kwa haraka.
 
Msolla mpaka aondoke ndipo Yanga itacheza mpira mzuri
Mnamuonea mzee wa watu bure tu, mimi nasema mpaka mashabiki mandazi kama nyie waondoke Yanga ndio mtacheza mpira mzuri, kila kocha anayekuja Yanga mfumo wenu huwa ni huo huo wa gombania goli, inapigwa pasi ndefu na kipa mpaka kwenye penalti box ya adui then mnaanza kuruka ruka mbahatishe kufunga, miaka yote hamuwezi kuanzisha mashambulizi kuanzia kwa kipa.
 
Pira Biriani. Pira Sambusa. Pira Soseji. Pira Chipsi Kuku na Kachumbari ya Mayor Naizi. πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯
 
Pira pilau la mawe, kachumbari ya miba juice ya maji ya betri 😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…