Kuanzia darasa la kwanza nilikuwa nachora, nilichora sana picha za darasani za kufundishia walimu waliponipa hio kazi.
Mfano wa picha ambapo nilichora when i was in primary school ni human evolution , hizo picha kwa ubora nilivyochora mwalimu wangu aliweka/kubandika kwenye ukuta nyuma ya darasa kwenye frame akawekea na lamination. Ajabu miaka ya karibuni nilienda hapo nikaikuta hio picha lile lile darasa nimesoma ni baada ya kupewa taarifa na rafiki yangu niliyesoma nae darasa moja ambae hivi sasa ana mtoto anasoma hiyo shule.
Kwa kumbukumbu zilizonirudia kidogo nilie baada ya kutizama ile picha iliyopo ukutani, nilikumbuka vingi sana, huyo mwalimu now ni marehemu, naamini kweli nilizaliwa na kipaji cha uchoraji, nimechora primary, secondary , advance hadi chuo.
Hivyo nikipata muda huwa nachora kwa sababu napenda, lakini nawaza kuja kufanya animations ya cartoons, hua najitafakari sana hiki kipaji changu siwezi kukiacha hivi hivi.