Huwa unamuamini asilimia ngapi mwenyeji wako anapokwambia usiogope, Mbwa wake hang'ati?

Huwa unamuamini asilimia ngapi mwenyeji wako anapokwambia usiogope, Mbwa wake hang'ati?

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Karibu sana mgeni! Usiogope Mbwa wangu hawang'ati!

Hii kauli huwa unaiamini asilimia ngapi ? Kuwa tu mkweli kabla sijakwambia jambo!
fad0f776eb323e9e-1024x681-2.jpg


Usisahau!

Kuna wanaong'atwa na mbwa wao wenyewe! Mfano kingunge, na mwingine south!
Screenshot_20230110-101052.png
 
Kuna nyumba moja niliwashangaa sana, niliingia nimefika uwani mbwa akakurupuka huko akanifata huku anabweka, nikaamua kutumia ujanja wangu, nikainama chini kama naokota jiwe mbwa anashituka kidogo ila tena asogea, wao wananiangalia tu, mbwa nae alikuwa jasiri sana nikimtishia kama namponda anatulia kidogo afu anasogea, eti baadae ndio wanakuja kumshika wakati huo nimeshachoka balaa nawaza sijui akinifikia kabisa itakuwaje
 
labda kama ufugi ila ukiwa unafuga unafahamu mbwa yupo vipi na ni aina gani.
ukiona mbwa anatingisha mkia kwa kuzungusha basi jua ni rafiki.ila ukiona mbwa atingishi mkia umesimama we jiamini kama umemkazia bila kuogopa.ukiona mkia kaushusha chini umeinama kwenye sehemu yake basi amekosa na aibu.

bahati nzuri nafuga hawa
9D60E193-B108-4CA5-BA28-889B1C432308.jpg
 
Kuna nyumba moja niliwashangaa sana,niliingia nimefika uwani mbwa akakurupuka huko akanifata huku anabweka,nikaamua kutumia ujanja wangu,nikainama chini kama naokota jiwe mbwa anashituka kidogo ila tena asogea,wao wananiangalia tu,mbwa nae alikuwa jasiri sana nikimtishia kama namponda anatulia kidogo afu anasogea,eti baadae ndo wanakuja kumshika wakati huo nimeshachoka balaa nawaza sjui akinifikia kabisa itakuwaje
Bahati mbaya wanang'ataga sehem nyeti na nyuma ya miguu!
 
Mzee kingunge alibadilishiwa mbwa mkuu ule ulikuwa mkakati wa kukiondosha kile kibabu.

kuna aina za mbwa inakubidi kuchukua vibari maana vizazi vyao vijatokana asili kubwa ya mbwa.

Kingunge alikuwa hafugi wala kulisha mlishaji na mfugaji alijasahau ndio kilichotokea.

Ingia google andika dangerous dogs type
 
Kuna jamaa nilienda kumtengenezea gari kwake. Kufika kwake nikakuta anafuga mbwa wawili, yan pit bull wakubwa walioshiba.

Akanambia wewe fanyakazi tu wala usiogope. Kwa vile ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika kwake, nikajifanya sina uoga na viumbe wale.

Nikiwa katika harakati zangu za kazi mara jamaa akanifuata na kuniambia kuwa anatoka mara 1 kwenda kumfuata mtoto shuleni (sio mbali sana na anapoishi) akasema wewe usiwe na wasi wasi hao hawawezi kukufanya chochote.

Dah kukataa nikashindwa na kukubali pia nikashindwa nikabaki kumeza fundo la mate huku nikijifanya sina wasi wasi na viumbe wale. Jamaa akaniachia funguo 1 ya gate la nje akafungua gate akatoka na kutuacha sisi watatu, yani mimi na ile mi pit bull miwili, basi ikawa inaniangalia huku inanikazia macho kama vile inataka nijichanganye kidogo tu inichane chane, maana tayari ulimi uko nje, huku mijino kama vidole vya mtu mzima.

Kitu cha kwanza nikatoka chini ya gari na kuingia ndani ya gari. Sasa wakati nikiwa ndani ya gari nikasikia honi ya gari inaita kwa nje ya nyumba, nikajiuliza huyo ni mshikaji amerudi anataka nikamsaidie vitu au ni mtu mungine anapiga honi nyumba ya pili, honi ikaendelea wale mbwa wakakurupuka na kukimbilia mlangoni wakawa wanabweka ile mbaya.

Hapo nikajua anaepiga honi yuko mlangoni na pia inaonesha sio mwenyeji wa nyumba ile maana ingekuwa ni mwenyeji wasingebweka vile, kidogo simu inaita jamaa ananambia nichukue funguo alioniachia nikamfungulie mgeni wake.

Hapo ndio palikuwa patamu maana jamaa nilikuwa nishamuonesha kuwa wale mbwa siwaogopi, sasa naanzaje tena kumwambia kuwa naogopa kwenda kufungua? Ikabidi nimwambie kuwa niko msalan nakata gogo, akasema poa fanya fasta basi ukamfungulie.

Jamaa akampigia akamwambia mgeni asubiri nikimaliza kukata gogo nitamfungulia. Baadae akanipigia tena bado tu, nikabidi nimwambia ndo najisafisha natoka sasa hivi.

Nikasema potelea mbali wakinivamia atanilipa, nikaanza kulifuata gate la nje kwa kunyata kumbe washanisikia ghafla nikaona hao wanakuja mbio upande wangu, nikaona nikikimbia watanivamia, ikabidi nioneshe ukakamavu ghafla hawa miguuni, sasa nilichofanya nikamshika yule dume kichwani kama nampalaza palaza likatulia huku likionesha kuelewa ninachokifanya nikawa natembea mdogo mdogo kuelekea getini huku wakinifuata kama vile ni mtu wanaenifahamu, ile kufika getini nafungua na mwenyeji namuona yule kwa mbali anakuja. Basi wakaingia wote mwenyeji, mtoto na mgeni tukafunga geti.
Aisee siku ile sintoisahau.

Kwa wale wasiomjua pit bull, huyu hapo pichani kulaleki 😂
 

Attachments

  • images (64).jpeg
    images (64).jpeg
    21.5 KB · Views: 10
Unaambiwa usiogope, Mbwa yupo miguuni anabweka, halafu mwenyeji hana habari anaingia ndani,
Na usiombee wawe wawili kuna mwingne anazunguka,

Unajiwa na ujasiri usipanick ila ujasiri haudumu, unaweza umtukane mwenyeji ukiona analeta utani na usalama wako.

Huwezi ukamuamini mwenye mbwa 100% mana yeye ndio mnafahamiana mbwa hakujui.
 
Asilimia 10 na kwenda chini.

Khaaa mbwa ana akili zake.. binadamu atajuaje hawezi kunitenda na mtu unajuwa nilikali haswaa... 😅😅😅
Sometimes unaweza kufikiri labda jamaa mwenye mbwa kanileta makusudi ili nije kuwa kitoweo cha mbwa wake.

Taratiib utaanza kusikia kiushuzi kinatoka chenyew huku ukipumua kwa namna isiyokuwa ya kawaida yako, na wakati huo mbwa nao wanaangalia movement yako ili ukijichanganya tu wakuoneshe kazi 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom