Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mim mambo ya mi mbwa sitaki kidg wanitafuneKaribu sana mgeni! Usiogope Mbwa wangu hawang'ati!
Hii kauli huwa unaiamini asilimia ngapi ? Kuwa tu mkweli kabla sijakwambia jambo!
View attachment 2453454
Mbwa akishakuwa karibu yako hautakiwi kukimbia, maana kitendo cha kugeuka ili ukimbie mwenzako atakichukulia kama vile unapanga shambulizi dhidi yake, so atakuwahi na atakuchana chana vibaya sana.Mimi ile wanakuja kwangu tu, ningeludi ndani ya gari mbio hahahaha
🤣🤣🤣 Mkuu pamoja na kwamba niliogopa ujio wao, lkn niliona sina njia nyingine ya kufanya ili nijinusuru ikabidi nijifanye tunafahamiana. Na wao kwa bahati nzuri wakanielewa.Wewe ni jasiri sana kwa hapo mimi ningeliwa tu mana ningetoka mbio na hili ni kosa. Mbwa sinaga urafiki nao kabisa wakati mtoto waliwahi kuniumiza hadi leo hii hawa viumbe hatuna ukaribu kabisa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nipe tip hyo ya nyukiKatika viumbe ambao huwa siwaogopi ni mbwa na nyuki nimecheza nao muda mrefu najua tabia zao sana nyuki akikutana na mimi huwa anageuka kipepeo na mbwa anageuka mbuzi
Hahaaaaambwa ambaye haumi wenyeji ulio nao hawezi kukuuma wewe,kosa la kwanza ni kuanza wenge kama unachomoka mabawa mgongoni na kukimbia hovyo ukitengana na wenyeji wako,atakuuma.
saikolojia ya mbwa hubadilika anapoona mgeni,lakini mgeni salama ni yule aliye na mwenyeji wake au aliye mtulivu hata baada ya yeye kubweka.
kuna mpuuzi nilienda naye nilipopanga kulikuwa na geti na mbwa,nikamtahadhalisha mbwa haumi,awe mtulivu heee,kufungua tu geti mbwa akamsogelea jamaa akaanza kutuka ruka kama kuku kavaa mvuko mguuni😂😂,mpaka ananirukia mimi,yaani nilimind sijui alikuwa na majini mjinga yule.
Mkwara huoAisee! Hakuna mnyama rafiki kama mbwa,mnyama yeyote ukurarua tu pale anaposikia harufu ya uoga wa MTU....kutikisika kwingiii...lakini ukijiamini nae anaogopa hawezi kukugusa.
Na kuhusu kuamini kauli ya mwenyeji ni kwamba kama aliongopa tu ili kuniaminisha bas nikiguswa ajiandae kuzika mbwa wake.
[emoji1][emoji1][emoji3][emoji3][emoji3]Nilishawah enda nyumba hivi mbwa hawaumi ila walinijaalia na kunizunguka nikawa naambiwa nisikimbie machoz yalinitoka sikuwah rudi pale tena
[emoji1][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]kiumbe ambae huwa ctakiii hata anisogeleeeKuna nyumba moja niliwashangaa sana, niliingia nimefika uwani mbwa akakurupuka huko akanifata huku anabweka, nikaamua kutumia ujanja wangu, nikainama chini kama naokota jiwe mbwa anashituka kidogo ila tena asogea, wao wananiangalia tu, mbwa nae alikuwa jasiri sana nikimtishia kama namponda anatulia kidogo afu anasogea, eti baadae ndio wanakuja kumshika wakati huo nimeshachoka balaa nawaza sijui akinifikia kabisa itakuwaje
Ungekimbia tu ungeisoma namba [emoji23][emoji23]Kuna jamaa nilienda kumtengenezea gari kwake. Kufika kwake nikakuta anafuga mbwa wawili, yan pit bull wakubwa walioshiba.
Akanambia wewe fanyakazi tu wala usiogope. Kwa vile ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika kwake, nikajifanya sina uoga na viumbe wale.
Nikiwa katika harakati zangu za kazi mara jamaa akanifuata na kuniambia kuwa anatoka mara 1 kwenda kumfuata mtoto shuleni (sio mbali sana na anapoishi) akasema wewe usiwe na wasi wasi hao hawawezi kukufanya chochote.
Dah kukataa nikashindwa na kukubali pia nikashindwa nikabaki kumeza fundo la mate huku nikijifanya sina wasi wasi na viumbe wale. Jamaa akaniachia funguo 1 ya gate la nje akafungua gate akatoka na kutuacha sisi watatu, yani mimi na ile mi pit bull miwili, basi ikawa inaniangalia huku inanikazia macho kama vile inataka nijichanganye kidogo tu inichane chane, maana tayari ulimi uko nje, huku mijino kama vidole vya mtu mzima.
Kitu cha kwanza nikatoka chini ya gari na kuingia ndani ya gari. Sasa wakati nikiwa ndani ya gari nikasikia honi ya gari inaita kwa nje ya nyumba, nikajiuliza huyo ni mshikaji amerudi anataka nikamsaidie vitu au ni mtu mungine anapiga honi nyumba ya pili, honi ikaendelea wale mbwa wakakurupuka na kukimbilia mlangoni wakawa wanabweka ile mbaya.
Hapo nikajua anaepiga honi yuko mlangoni na pia inaonesha sio mwenyeji wa nyumba ile maana ingekuwa ni mwenyeji wasingebweka vile, kidogo simu inaita jamaa ananambia nichukue funguo alioniachia nikamfungulie mgeni wake.
Hapo ndio palikuwa patamu maana jamaa nilikuwa nishamuonesha kuwa wale mbwa siwaogopi, sasa naanzaje tena kumwambia kuwa naogopa kwenda kufungua? Ikabidi nimwambie kuwa niko msalan nakata gogo, akasema poa fanya fasta basi ukamfungulie.
Jamaa akampigia akamwambia mgeni asubiri nikimaliza kukata gogo nitamfungulia. Baadae akanipigia tena bado tu, nikabidi nimwambia ndo najisafisha natoka sasa hivi.
Nikasema potelea mbali wakinivamia atanilipa, nikaanza kulifuata gate la nje kwa kunyata kumbe washanisikia ghafla nikaona hao wanakuja mbio upande wangu, nikaona nikikimbia watanivamia, ikabidi nioneshe ukakamavu ghafla hawa miguuni, sasa nilichofanya nikamshika yule dume kichwani kama nampalaza palaza likatulia huku likionesha kuelewa ninachokifanya nikawa natembea mdogo mdogo kuelekea getini huku wakinifuata kama vile ni mtu wanaenifahamu, ile kufika getini nafungua na mwenyeji namuona yule kwa mbali anakuja. Basi wakaingia wote mwenyeji, mtoto na mgeni tukafunga geti. Aisee siku ile sintoisahau.
Wangemgeuza kiteweoUngekimbia tu ungeisoma namba [emoji23][emoji23]