Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
HahahWenyeji wengine ukizongwa na mbwa wao wanacheka tu[emoji1787],
Mie mbwa akitaka kunizongo nakuwa mkali zaidi yake,tena kama kuna mawe nampiga,
Home nachekaga tu usiku watu wanavyokimbia kuogopa mbwa,wangejua mijibwa yenyewe inabweka tu wala haing'ati[emoji16]
Na waking'ata na sumu ndo baasKuna mshkaji wangu nilikua naendaga kwao na wana mbwa ila wanasema ni coco yani mchana hana madhara mpaka usiku na pale kwa mshkaji naendaga mara nyingi tu na mbwa huwa ananiona ila hanaga ile kumfuata mtu miguuni kama wanavyofanya mbwa wengine wakiona tu mgeni kaingia haoo wanamkimbilia
Huyu hakua na hizo mambo yani wewe ukiingia utamkuta kalala zake hana time na wageni,sasa siku moja usiku nilienda tena kwa mshkaji wangu tukawa tunacheki movie ndani baadae muda wa kuondoka tumetoka nje mbwa yupo kibarazani na pale nje kulikua na mabox mawili jamaa akaniambia nimsaidie kuingiza ndani yeye akabeba box moja akaingia ndani sasa ile nataka kubeba box mara simu yangu ikaita hapo mbwa ananichora tu,nilivomaliza kuongea na simu ndo nikabeba box niingize ndani yani ile nakaribia mlango tu naskia mbwa ananikimbilia anabweka akapeleka mdomo wake karibu na mguu dah nilikimbilia ndani mwili unasisimka yan ilibaki kidogo tu achomoe mnofu
Mradi utesek tu [emoji1787][emoji1787]Kuna nyumba moja niliwashangaa sana, niliingia nimefika uwani mbwa akakurupuka huko akanifata huku anabweka, nikaamua kutumia ujanja wangu, nikainama chini kama naokota jiwe mbwa anashituka kidogo ila tena asogea, wao wananiangalia tu, mbwa nae alikuwa jasiri sana nikimtishia kama namponda anatulia kidogo afu anasogea, eti baadae ndio wanakuja kumshika wakati huo nimeshachoka balaa nawaza sijui akinifikia kabisa itakuwaje
Kuna jamaa nilienda kumtengenezea gari kwake. Kufika kwake nikakuta anafuga mbwa wawili, yan pit bull wakubwa walioshiba.
Akanambia wewe fanyakazi tu wala usiogope. Kwa vile ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika kwake, nikajifanya sina uoga na viumbe wale.
Nikiwa katika harakati zangu za kazi mara jamaa akanifuata na kuniambia kuwa anatoka mara 1 kwenda kumfuata mtoto shuleni (sio mbali sana na anapoishi) akasema wewe usiwe na wasi wasi hao hawawezi kukufanya chochote.
Dah kukataa nikashindwa na kukubali pia nikashindwa nikabaki kumeza fundo la mate huku nikijifanya sina wasi wasi na viumbe wale. Jamaa akaniachia funguo 1 ya gate la nje akafungua gate akatoka na kutuacha sisi watatu, yani mimi na ile mi pit bull miwili, basi ikawa inaniangalia huku inanikazia macho kama vile inataka nijichanganye kidogo tu inichane chane, maana tayari ulimi uko nje, huku mijino kama vidole vya mtu mzima.
Kitu cha kwanza nikatoka chini ya gari na kuingia ndani ya gari. Sasa wakati nikiwa ndani ya gari nikasikia honi ya gari inaita kwa nje ya nyumba, nikajiuliza huyo ni mshikaji amerudi anataka nikamsaidie vitu au ni mtu mungine anapiga honi nyumba ya pili, honi ikaendelea wale mbwa wakakurupuka na kukimbilia mlangoni wakawa wanabweka ile mbaya.
Hapo nikajua anaepiga honi yuko mlangoni na pia inaonesha sio mwenyeji wa nyumba ile maana ingekuwa ni mwenyeji wasingebweka vile, kidogo simu inaita jamaa ananambia nichukue funguo alioniachia nikamfungulie mgeni wake.
Hapo ndio palikuwa patamu maana jamaa nilikuwa nishamuonesha kuwa wale mbwa siwaogopi, sasa naanzaje tena kumwambia kuwa naogopa kwenda kufungua? Ikabidi nimwambie kuwa niko msalan nakata gogo, akasema poa fanya fasta basi ukamfungulie.
Jamaa akampigia akamwambia mgeni asubiri nikimaliza kukata gogo nitamfungulia. Baadae akanipigia tena bado tu, nikabidi nimwambia ndo najisafisha natoka sasa hivi.
Nikasema potelea mbali wakinivamia atanilipa, nikaanza kulifuata gate la nje kwa kunyata kumbe washanisikia ghafla nikaona hao wanakuja mbio upande wangu, nikaona nikikimbia watanivamia, ikabidi nioneshe ukakamavu ghafla hawa miguuni, sasa nilichofanya nikamshika yule dume kichwani kama nampalaza palaza likatulia huku likionesha kuelewa ninachokifanya nikawa natembea mdogo mdogo kuelekea getini huku wakinifuata kama vile ni mtu wanaenifahamu, ile kufika getini nafungua na mwenyeji namuona yule kwa mbali anakuja. Basi wakaingia wote mwenyeji, mtoto na mgeni tukafunga geti. Aisee siku ile sintoisahau.
Aisee sio tu ningeisoma namba bali pengine leo hii ningekuwa naitwa marehem fulani, au wangeniachia ulemavu wa kudumu, maana hakuna mbwa mkali, hatari na mwenye nguvu kama pit bull. Huyo german shepherd mwenyewe akikutana na pit bull ujue siku hiyo hata wenye mbwa wao wenyewe watashindwa kuwaamua.Ungekimbia tu ungeisoma namba [emoji23][emoji23]
ZerooKaribu sana mgeni! Usiogope Mbwa wangu hawang'ati!
Hii kauli huwa unaiamini asilimia ngapi ? Kuwa tu mkweli kabla sijakwambia jambo!
View attachment 2453454
Hahaha bata nao sometimes wanazingua. Hata hawa tunaowafuga ukikaa vibaya ujue anakutoa nduki kulaleki.Kuna mbwa na Bata mzinga
Nikikutana na hivyo Vitu kwako siingii getini
Hahahhh noma mkuu 😂😂Ukute umevaa skonko ko ko ko mbwa yuko nyuma anaitaman miguuu
Kaka uje kwetu uje uchezee na huyu mbwa na umfanye kua mbuzi..tulimtoa line police akiwa mdogoKatika viumbe ambao huwa siwaogopi ni mbwa na nyuki nimecheza nao muda mrefu najua tabia zao sana nyuki akikutana na mimi huwa anageuka kipepeo na mbwa anageuka mbuzi
Kalio alizani linadondoka nahisiUkiambiwa hivyo usiamini kwa asilimia 100 nakumbuka niliambiwa hivyo na mwenyeji wangu baadae wakati naongea na simu nikashangaa yule dogi kanipiga jino kalioni tena kwa kuvizia ni dog anayeng'ata kimyakimya mwanzoni nilikuwa nashangaa huyu dog mbona anazungukazunguka nyuma yangu kumbe anatataka kuning'ata kalio hii leo hata nikienda kwa jamaa yule dog simpi nafasi ya kukaa nyuma yangu