Huwezi amini kwamba hawa nao ni wasomi wa UDSM wanasaka degree

Mvumilivu hula mbivu but hawa wamezidi hata wao hawafikirii kutafuta njia mbadala ya kujikwamua na hili tatizo,degree sio pen na karatasi tu cha msingi wajiongeze

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hata kama ni mabibo, haimaanishi kuwa watu wanalala katika mazingira hayo.
Kila chumba kina vitanda vitatu kwa ajili ya watu watatu kukaa. Kimoja kinakuwa hakina deka, na kingine kina deka. Mimi nimekaa kwenye hosteli za Mabibo na udsm.
Kiutaratibu, baada ya kufika chuo mwanafunzi analipia chumba chake...ukilipia unapewa godoro.
Hakuna mtu anayeruhusiwa kulala bila ya godoro.
Kinachotokea ni ufisadi wa wanafunzi wenyewe.... mtu hataki kulipia chumba chake bali anataka kubebwa. Ndio maana unaona wanalala mzungu wa nne. Wanabana matumizi kwa kuchangia gharama za chumba.
Huyo aliyelala juu hajalipia...amezamia tu. Kwa kuwa hao waliolala chini ni washikaji zake. Kwa maana wana haki ya kutumia chumba.
UKILIPIA CHUMBA 9AMBAYO KWA SIKU WAKATI NASOMA ILIKUWA SH.200/= ...UKISHALIPIA UNAPEWA UFUNGUO NA GODORO.
UKIONDOKA UNARUDISHA UFUNGUO NA GODORO...USIPORUDISHA UNAHESABIWA DENI NA LAZIMA ULILIPE KABLA YA KUMALIZA CHUO. MIMI NILIKUWA MWATHIRIKA WAKATI FULANI. NILILIPIA CHUMBA NA WAKATI WA LIKIZO FUPI SIKURUDISHA GODORO WALA UFUNGUO...KUMBE IKAWA INAHESABIWA NILIKUWA NAENDELEA KUKAA.
MWISHO WA SIKU NILIPOKUWA NAFUATILIA CHETI NIKAELEZWA NINADAIWA CHUMBA KWA WIKI 3...NIKAKUMBUKA KUWA SIKURUDISHA.
KWA HIYO NIKALIPA NA NIKAPEWA RISITA...NDIO WADENI AKASAINI KUWA SIDAIWI,,,,,\KWA HIYO KWA WASIOJUA HILA NA MBINU ZA WANAFUNZI WANAWEZA KUKUBALIANA NA PICHA HIYO NA YALIYOSEMWA NA MLETA MADA...LAKINI UKWELI NI HUU
1) KUKWEPA KULIPIA CHUMBA
2) KUTAKA KUBEBWA
3) KUZAMIA...AMBAO NDIO UFISADI UNAANZIA HAPO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…