Huwezi amini lakini ukweli bila NATO, Marekani anaiogopa Sana Urusi

Huwezi amini lakini ukweli bila NATO, Marekani anaiogopa Sana Urusi

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Tunaambiwa kuwa Marekani ndio taifa lenye nguvu kabisa hapa duniani.

Lakini ukiangalia kwa undani utaona pengine ni wingi wa silaha tu lakini sio ujasiri.

Ukiangalia matendo ya Marakani dhidi ya Urusi ndio utajua kweli Marekani anaiogopa Urusi.

Mgogoro wa Urusi na Ukraine Marekani anaionya Urusi isijaribu kuivamia Ukraine kwa sababu mbili,
Moja anasema Urusi atalipa gharama kubwa,gharama zenyewe ni vikwazo.

Mbili anasema itatokea Vita kubwa lakini anaanza kuwaomba NATO wawe wamoja ili kumkabili Urusi peke yake.

Sasa najiuliza kwa Nini kama Marekani ni superpower awategemee NATO kumkabili Urusi peke yake?

Kwa Nini asiseme Urusi usivamie Ukraine nami ntapigana na wewe kupitia Ukraine?

Kwani bila NATO Marekani peke hawezi kumkabili Urusi?

Marekani pia aliwahi kuwaomba NATO wakamtoe Assad wa Syria NATO hawakutoa ushiriakiano,Urusi akasema Assad haondoki na Urusi akapeleka jeshi kumlinda Assad Marekani akaondoka Syria.

Urusi aliivamia Georgia na kajitwalia abkhazia na Osettia,akavamia Ukraine na kujitwalia Crimea.

Yote haya Marekani alitoa onyo Kali lakini ama aliomba ushiriki wa NATO ambao kwa kweli jamaa wale ama hawapendi kuingia mgogoro na Urusi ama hawapendi tabia za Marekani za kuichokoza Urusi.

Maana yangu ni kwamba Marekani hawezi kuikabili Urusi bila NATO na anachoweza kuikabili Urusi ni vikwazo tu.
 
Kwa taarifa yako NATO, bila USA, ni jibwa koko tu, ila USA, bila NATO, bado ni mbabe tu, unakumbuka kipindi cha trump alipotaka kuiondoa nchi yake kwenye NATO?Kwa kulalamika kuwa mzigo mkubwa wa kufedha anaubeba yeye, nini kilitokea kwa viongozi wengine wa NATO?!Siasa za URUSI ni za kishamba sana, na kwa sasa hawezi kuachwa na kufanya anavyotaka kwa kutaka kulazimisha tena Umoja wa soviety!!ni mikwala tu, kwani juzi ameambiwa na USA ana option mbili tu kuivamia Ukraine, nakuwa tayari kulipa ghalama za uamuzi huo, au kuacha!!
 
Bila kushirikiana hakuna mafanikio .na kama kweli mrusi mbabe awapige ukraine .mjomba acha ushabiki wa simba na yanga . Liogope sana taifa la marekani kwenye kila Nyanja unayoijua wewe bila marekani hakuna Amani duniani ukubali ukatae ukweli ndio huo
 
Vita ni gharama, kama unaweza kupata wapambe wa kukuunga mkono kupunguza gharama basi unafanya hvyo.
Sema Marekani siku hizi anabweka sana bika kung'ata
Marekani sio wapuuzi kama unavyofikiri, wamwjipa muda wa kurekebisha uchumi ulioyumba kipindi cha Bush na Obama kidogo.

Mpango wao wa kuchagua wazee kwa vipindi 2 mfululizo ni mkakati wao kwani wazee hawana kazba.

Trumph hakupenda vita zaidi ya mikwara ndio maana alijishusha akaongea na Kiduku.

Biden ndio kabisaa hata kusikia vita, kwa ujumla Marekani imepoa.

Baada ya Biden rais ajaye atakuwa mtu wa makamo na hapo ndipo tutauona moto wake.
 
Bila kushirikiana hakuna mafanikio .na kama kweli mrusi mbabe awapige ukraine .mjomba acha ushabiki wa simba na yanga . Liogope sana taifa la marekani kwenye kila Nyanja unayoijua wewe bila marekani hakuna Amani duniani ukubali ukatae ukweli ndio huo
Ni washenzi mno hawa watu
 
Marekani sio wapuuzi kama unavyofikiri, wamwjipa muda wa kurekebisha uchumi ulioyumba kipindi cha Bush na Obama kidogo.
Mpango wao wa kuchagua wazee kwa vipindi 2 mfululizo ni mkakati wao kwani wazee hawana kazba.
Trumph hakupenda vita zaidi ya mikwara ndio maana alijishusha akaongea na Kiduku.
Biden ndio kabisaa hata kusikia vita, kwa ujumla Marekani imepoa.
Baada ya Biden rais ajaye atakuwa mtu wa makamo na hapo ndipo tutauona moto wake.
Anahaha Mchina kamkalia kooni uchumi wake sasa hivi unapaa. Ndani ya miaka kadhaa ijayo mchina atakuwa anaunda kila kitu.
Sasa hivi anabweka tu kwasababu vinchi vinabshana nae
 
Anahaha Mchina kamkalia kooni uchumi wake sasa hivi unapaa. Ndani ya miaka kadhaa ijayo mchina atakuwa anaunda kila kitu.
Sasa hivi anabweka tu kwasababu vinchi vinabshana nae
Tatizo mchina tayari ana jina baya kuhusu bidhaa zake, hili ni tatizo kubwa hivyo hawazi kuwa mshindani hatari kwa Marekani.
 
Tatizo mchina tayari ana jina baya kuhusu bidhaa zake, hili ni tatizo kubwa hivyo hawazi kuwa mshindani hatari kwa Marekani.
Ana jina baya wapi? Umesahau kuwa electronics za majumbani za US zilikuwa manifactured China, China ana labor power ambayo ni skilled ndo maana hata makampuni mengi ya marekani ya prefer production ifanyike china.

Leo, imetoka report ya kitengo cha upelelezi cha germany ikisema kuwa hakuna ushahidi wowote kuwa simu za xiomi zinadukua mawasiliano ya watu.

Marekani ana propaganda tu kaona mchina anataka mpiku kaanza propaganda za kumchafua, kwani yeye hadukui watu?
 
Ana jina naya wapi? Umesahau kuwa electronics za majumbani za US zilikuwa manifactured China, China ana labor power ambayo ni skilled ndo maana hata makampuni mengi ya marekani ya prefer production ifanyike china.
Leo, imetoka report ya kitengo cha upelelezi cha germany ikisema kuwa hakuna ushahidi wowote kuwa simu za xiomi zinadukua mawasiliano ya watu.
Marekani ana propaganda tu kaona mchina anataka mpiku kaanza propaganda za kumchafua, kwani yeye hadukui watu?
Wewe kweli zuzu, niambie ndege ya abiria ambayo ina-operate duniani aliyoundwa China? Yaan America miaka ya 50 washaunda ndege za abiria China 2022 bado, niambie China Technology company ambayo inaweza kuzizidi Apple, Amazon na Google, bajeti ya USA ya jeshi ni Mara 10 ya China, US Noma sana
 
Back
Top Bottom