Huwezi amini sasa hivi JF hakuna mada nyingi wala Vibe la Simba na Yanga kama zamani

1.Simba na Yanga

2.Wasanii bongofleva na bongo muvi

3.Dini za mchongo
mitume/manabii/mapastor wa uongo..mafuta ya upako

4.kuzusha matukio kikombe cha babu loliondo,popobawa,..kushikwa bega kuibiwa nyeti,..nguvu za kiume..matukio ya kutengeneza kuhamisha mijadala.

5.Mazindiko kuwapumbaza kukimbiza mienge MWENGE

6.Machawa=wanafiki= njaa kali inayopelekea kujiuza+ kuuza utu wao.
 
Tanzania haitakaa irudi kama zamani kamwe, kama kulikuwa na mazuri ndio byebye, na kama yalikuwa mabaya basi hayatabaki kama yalivyokuwa hapo mmwanzo
 
Kaka niache kidogo😅😂
 
Watu wameanza kuvipotezea taratibu kadiri muda unavyoenda
 
Mimi mtazamo wangu ni tofauti kidogo kiufupi tangu jf ifungiwe uchangamfu wa uanzishashi wa mada na uchangiaji wa mada umepungua sana bila kujali ni jukwaa gani kiufupi majukwaa yote yamepooza sana sijui wachangiaji wengi waliuawa ni ngumu kujua ni kipi kinacho sababisha hili.

Jf ya sasa sio kama jf kabla ya kufungiwa imepooza mno japo kuwa imesaidia kupunguza mada za hovyo humu ndani.
 
Kweli siku hizi hakuna mada za hovyo kama Zamani 😂 😆
 
Reactions: ITR
Oya dogo adriz sasa ndio jina gani hilo kwenye hii ID 😆😅🤣😂
 
Huu msimu simba na yanga zinepoteza sana ushawishi.

Picha linaanza wote wametoa jezi mbaya

Injinia akaja kualibu kwenye harambee ya CCM kutumia brand ya timu kupata political mileage

MO29 nayo ikawa mwanzo wa habari za mpira na mziki kutopewa kipaumbele

Baada ya hapo ikaja afcon, na sasa hivi macho ya watu wa mpira yapo world cup
 
Hakika huku uswahilini ndio bado kunan maamuma wanajadili huo ungese wa simba na yanga
 
Kiufupi tupo kipindi cha reformation kwenye mindset zetu since October 29
Sifuatilii mechi yeyote ya Vigagula wa CCM Simba na Yanga wala sina mood kuhusu siasa ndio kabisaa nipo mbali now hata JF na log mara mbili kwa wiki basi kiufupi hii nchi haitakuja kurudi zama zile za uchangamfu na vibe za kiwaki tena!
 
Mimi sasa hivi ndo hata sijui ligi kuu inaendeleaje, kinara wa magoli ni nani. Mechi za hsimba na yanga nikizoangalia msimu na derby zao wenyewe na zile za caf champions league tu
 
Mimi sasa hivi ndo hata sijui ligi kuu inaendeleaje, kinara wa magoli ni nani. Mechi za hsimba na yanga nikizoangalia msimu na derby zao wenyewe na zile za caf champions league tu
Mimi mengi najikuta nayajua baada ya kuingia Insta na hiyo ni kwasababu tu ya Azamsports.

Maana wale chawa wote sijui Kisugu na wajinga wenzake wote niliwafichia white mapema kaba hata ya M029.

Club ilikuja kufuata baadaye after M029 nikaiminyia chekundu.

Kuna zile suggestions tu ambazo zimekuwa ziki show up kwenye feed kutokana na kuwa na kwenda viral pamoja na kuwa engaged na baadhi ya watu ambao wapo kwenye list yangu.

Kwa hiyo hata leo nisikie Simba wanacheza upenuni au nyuma ya kibaraza hapa kwetu bado sitoki kuangalia.

Nilivyoanza hii harakati wanangu wa mtaani walijua mzaha lakini saizi wameanza kunielewa kuwa nilimaanisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…