Huwezi amini Wazungu ndio wanalisha Hoteli za Kitalii Tanzania, Hii aibu kuu

Umeongea point kubwa sana. Wanachotuzidi wenzetu cha kwanza ni mtaji, cha pili maarifa na cha tatu ni consistency na cha nne discipline. Biashara ya mbogamboga anayosema mtoa mada hata mtanzania anaweza kuifanya akiwa na hivyo vitu nilivyovitaja hapo juu.

Wenzetu haswa wamiliki wa mahoteli wanahitaji consistency and quality supply. Unakuta hotel kama Verde wanakuambia wanataka kuku wa nyama wenye kilo mbili na 500 kila wiki. Kuweza kulihudumia soko hilo unatakiwa uwe na uwezo wa kutoa kuku wenye viwango hivyo wakati wote. Hapo ndio inabidi muingie mkataba ili kila mtu afanye kazi yake kutokana na terms and conditions za mkataba. Ununuzi wa aina hiyo unafanywa pia na makampuni kama KFC, Supermarkets, Balozi au shule kama IST.

Tatizo linakuja sisi mitaji hatuna. Mfano nyanya mtu analima msimu kwa msimu kwa hiyo anashindwa kukidhi soko la hoteli za kitalii maana wao mikataba yao ni kuwauzia kiasi fulani cha mboga kila wiki.

Sisi tunakosa hivyo vigezo vya ubora na consinstency. Muuzaji anashindwa kuzalisha kwa wakati kwa visingizio vingi mara mtaji umekata mara mvua zimekata sijui vibarua wanatega yaani hapo ndipo MZUNGU anatupiga bao.

Unavyoona watu wanalima mboga mboga mtaani usidhani wanaweza soko la mahoteli ambapo wana taratibu zao mzigo uje umenyooka na pia kuwe na muda maalum wa kusambaziwa bila kukosa

Ndhani mmeelewa tunafeli wapi
 
Uko sahihi sana boss. Nimeshuhudia kwa mzungu mmoja maeneo ya Ifunda, ana kampuni inayoitwa Masifio. Jamaa anapanda mboga kila wiki japo ni kwenye eneo dogo tu. Mazao kama nyanya na matango anapanda kwenye green houses lakini mengi anapanda kwenye open space. Kiukweli analima mboga aina nyingi sana ikiwemo na uyoga.
Ambacho jamaa kafanikiwa zaidi ni aina ya wateja alionao. Kama ulivyobainisha, wateja wake ni supermarkets kubwa, hotels kubwa na watu binafsi (hasa wazungu wenzake). Jambo la msingi analofanya ni kugrade mazao yake na kuyaweka kwenye packages makini. Anaweza kuvuna karoti kilo ishirini ila first grade ikawa kilo tano. Ana certificate ya kuwauzia baadhi ya mazao KFC na supermarkets kama Butchers, Shopper's n.k.
Wana online platform ambako mtu yeyote anayehitaji bidhaa zake anaweza kufunguliwa account. Kila mwisho wa wiki wanatangaza mazao waliyonayo kwa wiki itakayofuata, na wateja huweka order zao mapema. Kwahiyo, anavuna kulingana na orders.
Kuna mengi sana lakini atakayependa kujifunza zaidi anaweza uliza. Haitumiki teknolojia ya ajabu hata na hana wataalam wa ajabu, ni cheap labourers tu na wenye shule wachache. Naamini hata sisi tunaweza tukiamua kuzingatia details muhimu kama mdau alivyosema hapo juu.
 
Uwezo wetu ni mdogo sana kuhusu kilimo cha kisasa, ndhani hapa ndio Mh Bashe angesimamia hawa wazungu wakulima wapo wengi tu hapa tanzania wanamiliki maeneo makubwa mpaka utashangaa, wengine wanafuga ng'ombe ambao hapa Tanzania ni wao tu wanao na pia kuna wengine wanafuga kuku na hao wote soko lao ni mahoteli makubwa ya watalii huko mbugani na maduka makubwa ya vyakula hapa Afrika ya Mashariki, wanaaweza hivyo sababu wao wana uwezo mkubwa wa mitaji, hawategemei mbolea na pembejeo za hati fungate sijui hati za ghala au Amcos, wanajua wanafanya nini wanalima kisasa kwenye magreen house ,wana matractor wana mabwawa kwa ajili ya kumwagilia mazao yao,hawategemei mvua za msimu, wana maloli yenye kuhifadhi ubaridi, malori yanatoka iringa hadi Airport na mzigo kwenda Zanzibar au huko Arusha sasa sisi unategemea usafirishe nyanya na fuso lililowazi, mazao yao yana kiwango cha kimataifa, na mwisho mzungu anamwamini mzungu mwenzake- ukitaka kuamini hilo utashangaa unapoona mzungu anaenda hoteli ya mzungu mwenzake ambayo hata haina sakafu ya marumaru wala swimming pool ukilinganisha na hoteli ya mzawa mweusi ambaye ana bonge la hoteli kulinganisha na hoteli ya mzungu.pale Mbeya na Songwe wakulima wakubwa wa kahawa ni wazungu na wamarekani weusi, hao ndio pia wenye migahawa mikubwa ya kahawa jijini Dar,Arusha na Zanzibar hawa ndio wanauza kahawa yao Marekani,Ujerumani na nchi nyingine za bara la Ulaya, wanapoamua kulima au kufanya biashara tayari wanakuwa wamekuwa na soko,tofauti na sisi ukilima mahindi au mpunga wako huruhusiwi kuuza nje,serikali inakuamulia lakini kwa hawa wazungu serikali haiwagusi kwa kuwaita ni wawekezaji, wakati si kweli wengi wao wamezaliwa hapa hapa baba zao walikuja miaka ya 50s na wengine wapo hapa hasa kuanzia miaka ya 90 walikuja kama watalii wengine kama wafanyakazi kwenye maofisi mbalimbali na waliweza kununua maeneo makubwa kwa pesa kiduchu na sasa ni matycoon, hawa hutawaona kwenye mikutano ya kisiasa bali utakuta viongozi wetu ndio hufanya ziara za''mafunzo'' kwenye mashamba yao mara utawaona wajumbe wa kamati za bunge wakifanya ziara huko mashambani na sijui wanajifunza nini.
 
Tatizo letu sisi kila kitu ni politicalized na ubabaishaji mwingi kilimo ni jambo kubwa na lenye kuhitaji seriousness kitaifa lakini serikali imeingiza siasa matokeo yake hakuna la maana sera bila vitendo ni bure, hizo biashara green house akifanya mswahili ile serious utaona maofisa wa mamlaka husika watakavyomsumbua.

Mfano; wewe mzawa fungua tu kiwanda kidogo uone usumbufu utakao pata wakati unafanya shughuli zako mara kwa mara maofisa wa Nemc,Osha, Tra,Tbs,Tmda, halmashauri nk kutwa wanakuja kutafuta kasoro ili uwaonge na ukishaanza waonga basi tayari unakuwa ni mrija wao wa kujipatia pesa... lakini same business akifanya mgeni hapati usumbufu huo kabisa... wanaogopa
 
Sina cha kuongeza umemaliza kila kitu, lakini kwa wazungu wala huwaoni halafu wazungu wanawatumia sana wenyeji masikini kuwafanyisha kazi ngumu kwa malipo kidogo sana na hugeuka wao kama ndio wanawasaidia hao wenyeji, huku kuna uonevu mkubwa na hizo mamlaka ulizozitaja wakienda kumuona mzungu huufyata na kuambulia kupiga nao picha. Kwa wazawa nchi hii ngumu sana kufanya si kilimo au biashara tu bali kila jambo, wenye mamlaka warasimu sijapata kuona.
 
ukweli mchungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…