nokwenumuya
JF-Expert Member
- Jun 29, 2019
- 820
- 2,896
Katika jamii mbalimbali za Africa na hata kwenye biblia ilikuwa ni sehemu ya tamaduni kwa mdogo mtu kurithi mke wa kaka yake pindi kaka yake anapotokea kufariki dunia.
Lakini katika kutimiza mila hizo hakukuwa na harusi, sherehe, shamrashamra, kukusanya watu, kuvipa vyombo vya habari pesa ili visambaze sherehe hizo za mtu kumrithi mke wa Marehemu kaka yake.
Walikuwa hawafanyi hivi sababu ya huzuni ya kuondokewa na kaka yao.
Lakini ukiona mdogo mtu anaitisha harusi na kutaka kusifiwa kwa kumrithi mke wa kaka yake mwaka mmoja, miwili na kuendelea kwa sherehe na wakati tulimuamini auguze mgonjwa basi inatupa tafsiri kwamba huyu mdogo mtu wakati wa kumuuguza kaka yake itakuwa alimhujumu na ndio maana anasherehekea kifo cha kaka yake wala hana huzuni wala jitihada za kukumbuka kifo cha kaka yake.
Haya mambo katika tamaduni hayajawahi kutokea. Hivyo tunaamini mdogo wetu alikuwa sehemu ya kumuua kaka yake.
Kwa kuwa kushiriki mauaji ya kaka yake na kufanya sherehe ni laana basi hataishi kwa amani na mke atakayemrithi hata atumie kiasi gani cha pesa alizorithi kwa kaka yake kutafuta wapambe wa kumsifia wala kuvipa pesa vyombo vya habari kumsifia maana sisi ndugu wa Marehemu kaka yake tunaona huo ni ukiukaji wa mila na hakika mwisho wake ni mbaya sana. Ukiua kwa Upanga.