Huwezi kufanya sherehe ya harusi kwa mke wa kurithi kama hukuhusika na kifo cha kaka yako

Katika jamii mbalimbali za Africa na hata kwenye biblia ilikuwa ni sehemu ya tamaduni kwa mdogo mtu kurithi mke wa kaka yake pindi kaka yake anapotokea kufariki dunia.

Lakini katika kutimiza mila hizo hakukuwa na harusi, sherehe, shamrashamra, kukusanya watu, kuvipa vyombo vya habari pesa ili visambaze sherehe hizo za mtu kumrithi mke wa Marehemu kaka yake.

Walikuwa hawafanyi hivi sababu ya huzuni ya kuondokewa na kaka yao.

Lakini ukiona mdogo mtu anaitisha harusi na kutaka kusifiwa kwa kumrithi mke wa kaka yake mwaka mmoja, miwili na kuendelea kwa sherehe na wakati tulimuamini auguze mgonjwa basi inatupa tafsiri kwamba huyu mdogo mtu wakati wa kumuuguza kaka yake itakuwa alimhujumu na ndio maana anasherehekea kifo cha kaka yake wala hana huzuni wala jitihada za kukumbuka kifo cha kaka yake.

Haya mambo katika tamaduni hayajawahi kutokea. Hivyo tunaamini mdogo wetu alikuwa sehemu ya kumuua kaka yake.

Kwa kuwa kushiriki mauaji ya kaka yake na kufanya sherehe ni laana basi hataishi kwa amani na mke atakayemrithi hata atumie kiasi gani cha pesa alizorithi kwa kaka yake kutafuta wapambe wa kumsifia wala kuvipa pesa vyombo vya habari kumsifia maana sisi ndugu wa Marehemu kaka yake tunaona huo ni ukiukaji wa mila na hakika mwisho wake ni mbaya sana. Ukiua kwa Upanga.
Afrika yetu hii
 
Kweli hizi mila za kurithi bila kupitia mchakato wa kuchumbia hazifai maana unapata mume mwenye uwezo mdogo wa kuendesha familia hatimaye madawa ya kulevya yanakuwa kwa wingi nyumbani na kuathiri watoto. Hatimaye mali za familia zinachukuliwa kiholela na wezi aliowadhibiti kaka.
Fanyeni maandamano,
 
Ndio inatakiwa wapewe ubini wa Marehemu sio kujifanya wapya
Marehemu ndo katungisha mimba? Aliyekufa kafa jamani, maisha lazima yaendelee, mke atarithiwa na atapewa mimba nyingine, watoto alowaacha watamtii na kumuita Baba huyo aliyemrithi mama Yao.
 
Naona sukuma gang wanampiga mafumbo bi shungi wakati wanajua kabisa mama hizo lugha ni sehemu ya utamaduni wake. Tukubali tu kuwa imeshatokea na yameshapita hayo mambo.
 
Katika jamii mbalimbali za Africa na hata kwenye biblia ilikuwa ni sehemu ya tamaduni kwa mdogo mtu kurithi mke wa kaka yake pindi kaka yake anapotokea kufariki dunia.

Lakini katika kutimiza mila hizo hakukuwa na harusi, sherehe, shamrashamra, kukusanya watu, kuvipa vyombo vya habari pesa ili visambaze sherehe hizo za mtu kumrithi mke wa Marehemu kaka yake.

Walikuwa hawafanyi hivi sababu ya huzuni ya kuondokewa na kaka yao.

Lakini ukiona mdogo mtu anaitisha harusi na kutaka kusifiwa kwa kumrithi mke wa kaka yake mwaka mmoja, miwili na kuendelea kwa sherehe na wakati tulimuamini auguze mgonjwa basi inatupa tafsiri kwamba huyu mdogo mtu wakati wa kumuuguza kaka yake itakuwa alimhujumu na ndio maana anasherehekea kifo cha kaka yake wala hana huzuni wala jitihada za kukumbuka kifo cha kaka yake.

Haya mambo katika tamaduni hayajawahi kutokea. Hivyo tunaamini mdogo wetu alikuwa sehemu ya kumuua kaka yake.

Kwa kuwa kushiriki mauaji ya kaka yake na kufanya sherehe ni laana basi hataishi kwa amani na mke atakayemrithi hata atumie kiasi gani cha pesa alizorithi kwa kaka yake kutafuta wapambe wa kumsifia wala kuvipa pesa vyombo vya habari kumsifia maana sisi ndugu wa Marehemu kaka yake tunaona huo ni ukiukaji wa mila na hakika mwisho wake ni mbaya sana. Ukiua kwa Upanga.
Jiwe gizani, watakurupuka huko mazima waanze mentioning wakati hakuna alotajwa names humu.
 
Back
Top Bottom