Huwezi kujua ubaya wa kutawaliwa na CCM mpaka ujue kinachoendelea Kenya

Huwezi kujua ubaya wa kutawaliwa na CCM mpaka ujue kinachoendelea Kenya

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Siyo kwamba Wakenya ni tofauti Sana na wananchi wa nchi nyingine Afrika bali angalau wao Kila wakati wanaweka rekodi kuelekea jamii huru na yenye watu wenye utimamu wa akili.

Hebu jiulize:

Vyuo Vikuu vya Kenya vimezalisha kizazi cha Gen Z kilicho makini na chenye kupigania usawa kwenye nchi yao. Wakati vyuo vikuu vya Tanzania vinazalisha watu wa aina ya Mwijaku..

Mahakama ya Kenya iliwahi kufuta uchaguzi wa Rais, hapa kwetu mahakama imechukua miaka zaidi ya mitatu kujua tu Kama kina Halima Mdee wapo kisheria Bungeni ama lah!

Ukiona unafurahia CCM kuwepo madarakani, jua wewe ni yule mmoja kati ya wale watanzania wanne.
 
Watanzania wengi ni mazezeta sababu kubwa ni CCM.

Nyerere aliangamiza hi nchi kwa ujamaa uchwara.

Mkapa na Kikwete wakairudisha nchi kwenye reli, akaja Magufuli ndyo akaizika kwa udikteta uchwara.

Ukifanya tasmini ya haraka majimbo yaliyokuwa yanaongozwa na upinzan yalipata mwamko wa maendeleo
 
Kikubwa hao walipata uhuru kwa kupambana ,huku uhuru ulipatikana mezani, like father like son🦅
Kwa ivo Hilo tu ndilo linalofanya tusifanane baada ya Uhuru wetu zaidi ya miaka 60 iliyopita!!??
 
Kuachana na ccm tu..ni ngumu sana kutambua mbongo anataka nini..? Muda wote ana shida ukijaribu kumtatulia atakubeza tena.,,kwa kifupi kila mtu abebe msalaba wake na familia yake...ikifika uchaguz vijana utazani wanaishi America..,full uchawa
 
Dah yani kuwatoa ushindwe sawa,, ila na pesa zao usizile jamani, kula lazima ila kura tutajuana mbele kwa mbele
 
Back
Top Bottom