Huwezi kumiliki/ kumilikishwa/ kuendesha LC 300 kama hutumii nguvu za giza

Hapo ndipo tofauti ya sisi na akina Bhakressa ilipo! Ila kuna raia wanakaza ubongo tu.

Fumbo la kiimani hilo!
 
Yamkini mazingira uliyokulia ndiyo yamekukutanisha na hayo, maana wanasema ukiwa rafiki na mwizi hata we unaweza kuwa mdokozi, nimeishi maisha ya mjini sijawahi Kutana na huu upumbavu wa kishirikina, watu wenye fikra za ushirikina wengi wanatokea vijijini. Zunguka kwenye miji ya watu walipendelea huo upumbavu huukuti na bado watu wana pull mandinga hatari ya mabosi wao.
 
Mganga ni Connection tu kama hauna Connection sahihi utaenda vijiji vyote na hakuna kitu utapata zaidi ya kupoteza nauli na wazee kula kuku zako na mbuzi..
 
Kwaiyo wazungu wakifanikiwa huwa wanaona wamefanikiwa kwa nguvu ya nani?
 
Waganga wenyewe hawazitaki hizo hela, wanawaachia ambao hawajui madhara yake na waliojawa na tamaa.

Wanatamba nazo lakini mwisho wao hauwezi kuwa mzuri.
Mwisho wetu sote hauwezi kuwa mzuri kwasababu wote mwisho wetu ni kufa au kuzeeka Kisha kufa na hivyo vyote sio vizuri kwa mwanadamu
 
Umeishi mji upi?nimezaliwa DSM enzi za Nyerere,hakuna sehemu kuna ushirikina kama kariakoo,usione maduka yale ukadhani yspoyapo tu,wapemba,wakinga ni noma kariakoo ni jehanam kabisa

Asubuhi nenda Azania front au KKKT kariakoo,kuna ibada za asubuhi,wale sio wajinga kumuomba Mungu,kuna vita ya kiroho sana huko maofisini hata hao wasomi wanarogana mno,huwezi kuamini ila ndio hivyo,madereva wa STK waogope
 
Kikundi kimoja cha nyimbo za kumsifu mungu kiliwahi kutoa kibao kimoja kinaitwa "Mchanganyo"

Ukiisikiliza vyema hiyo kwaya utapata maana sahihi ya kauli yako ndugu Mdukuzi, naungana nawe na nimekuelewa vizuri Sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…