Huwezi kuona uzuri wa Tanzania ukiwa Tanzania

Huwezi kuona uzuri wa Tanzania ukiwa Tanzania

Ume

Umeenda LONDON,lakini ujinga haujakutoka,........yamkini umeenda kuongeza upumbavu.
1. Enhe kati ya London ambapo chips ni elfu 55 na Tanzania wapi ni rahisi kuipata hio elfu 55?
2.Kua London na Tanzania kote daktari,dereva,mwalimu etc wanalipwa mshahara sawa?
3.unaweza weka average payment per hour ni London as compared to Tanzania,in term of any currencies in this world?
4.Per capital ya London na GDP ni kiasi gani na ya Tanzania ni kiasi gani?
Ukijibu hayo maswali wit references,utaweza kua mjinga
Naweza kukuelimisha jambo. Uingereza pamoja na mambo yote Lakini bado nitasema watu Wana suffer kuaccess huduma bora. Malazi kwao ni issue. Gharama ya Maisha iko juu. Hata chakula tu ambacho ni basic need kule siyo rahisi kuaccess. Pato la taifa ni kubwa ukilinganisha na Tanzania lakini Watu ni masikini kwasababu kuna Mabwenyenye wachache wamemiliki uchumi wa nchi na kusababisha wabust pato lao la taifa ambalo pia hufanya Pato la mtu mmoja mmoja kuwa kubwa.

Unaweza kujiona una kazi nzuri unalipwa mshahara mzuri lakini badae mshahara wote unaishia kwenye Kodi, chakula, kulala na usafiri. Kifupi unafanyia tumbo. Ndiyo maana ni nadra sana kukuta mzungu kajenga nyumba lakini Tanzania ni kawaida kijana mdogo kumiliki bonge la hekalu kwahiyo tusijitoe akili.
 
Kuna vitu umezungumzia.
1. Uaminifu.. basi tungependa viongozi wetu wawe waaminifu, matumizi ya pesa yaheshimiwe, waziri wa fedha huko anaenda bungeni na kausafiri simple, sisi kwetu huku, anaenda na escort si mchezo.
UWAJIBIKAJI tatizo kwetu, hatuna huduma bora, kuanzia afya, miundombinu, elimu etc.

2. Huyo msomali aliyekwambia usilinganishe pesa ya madafu ya tanzania na ya huko sawa sawa.. pesa yetu haina thamani..
Angalia pauni moja, kwetu ni tsh 3500 huko, achana na majina ya pauni ma shilingi, zote tuite pesa,
Yaani pesa yao 1 kwetu sisi ziwe 3500.
Akitaka kitu cha pesa 1, sisi kwetu uwe na pesa 3500 😂🤣
Shida hapo pesa yetu haina thamani.

Vipi ulijaribu kulinganisha huduma za KIJAMII na UBORA wake... elimu na mengineyo?

Tuache uzombi sisi tupo 50 kweusi, bado tunaishi hovyo, sikatai na sipingi kula misosi asilia, hapa naenjoy sana..
Lakini je hili pekee ndio la kujivunia.
Unajua sasa hivi kuna mbegu za mahindi 🌽 bongo, ukipanda, ukavuna hayo mahindi huwezi tumia yena kama mbegu, kama hujui basi ndio ujue na unakula.

Vipi mshahara wa mwalimu, daktari huko ni pesa ngapi za huko, na huku ni pesa ngapi kwetu?

Kama tungekuwa makini, viongozi wetu wangekuwa na nidhamu maali za taifa hili, huruma kwa watanzania, tusimgekuwa hapa tulipo.

Mwaka 2025 hii kuna mtanzania analimia jembe, vipi huko uingereza wanalimia majembe bado.
Ama kulimia jembe nako ni ufahari!?
 
Naweza kukuelimisha jambo. Uingereza pamoja na mambo yote Lakini bado nitasema watu Wana suffer kuaccess huduma bora. Malazi kwao ni issue. Gharama ya Maisha iko juu. Hata chakula tu ambacho ni basic need kule siyo rahisi kuaccess. Pato la taifa ni kubwa ukilinganisha na Tanzania lakini Watu ni masikini kwasababu kuna Mabwenyenye wachache wamemiliki uchumi wa nchi na kusababisha wabust pato lao la taifa ambalo pia hufanya Pato la mtu mmoja mmoja kuwa kubwa.

Unaweza kujiona una kazi nzuri unalipwa mshahara mzuri lakini badae mshahara wote unaishia kwenye Kodi, chakula, kulala na usafiri. Kifupi unafanyia tumbo. Ndiyo maana ni nadra sana kukuta mzungu kajenga nyumba lakini Tanzania ni kawaida kijana mdogo kumiliki bonge la hekalu kwahiyo tusijitoe akili.
Umetembea bongo lakini, watu wanakunywa maji yale yale wanayokunywa punda na ng'ombe.

Kijana analima heka kwa 70k mpaka laki!?

Ona aibu mkuu, acheni kuendekeza uchawa..
Maisha ya mtu wa kati na chini ni mateso mazito.
Kipi bora upate kazi pesa yote iishie kwenye, malazi, makazi, uweze kumudu huduma za afya
Ama ufanye kazi na bado hatabkula yako ya mbinde?

Una miliki shamba, ama ushawahi kwenda shamba bongo ama vijijini ukawaona wanavyotaabika, kisa elfu 5!?
Acheni hizo, tupaze sauti kuna watubwa chini wanataabika... Mkuranga tu hapo lami changamoto na huu ni mwaka wa 60+ toka tupate uhuru.
Mama mjamzito anajifungulia njiani kweli..!!
 
Lundo la MAANDISHI.


Maandishi kama 6,000,000,000,000.


Anyway, Tunawachukia WANASIASA kwasababu wanataka kuharibu NCHI.

Tungekuwa hatuipendi nchi yetu wala tusingehangaika na hao wanasiasa watawala unaowataja.
 
Waafrika tunakasumba ya kuwaona wazungu wanaoishi Ulaya kama watu wenye maisha mazuri kuliko Waafrika wanaoishi Afrika. Tumeitukuza Ulaya na Wazungu wanaoishi huko kuliko waafrika wanaoishi Afrika. Wazungu wamejitahidi kujipamba na kujipambanua kwa Waafrika kuwa Ulaya ni kuzuri na kuna maisha mazuri kuliko Afrika huku ukweli ukiwa tofauti kabasi. Afrika na hasa Tanzania inayoongozwa na Rais wetu Mhe. Dokta Samia Suluhu Hassan, kuna maisha mazuri na rahisi. Kila kitu unachotaka kula kinapatikana kirahisi, bei nafuu na tena kikiwa freshi. Lakini ukiwa Tanzania huwezi kuyaona maisha hayo hadi upate bahati ya kwenda kwao huko uone maisha yao na namna wanavyoishi.

Wazungu wanahaha asikuambie mtu, maisha kwao ni magumu si kawaida, vitu ni ghali na vilevile kodi iko juu. Kuna watu wanatuaminisha kuwa Tanzania kuna maisha Magumu mara tuandamane, tulete vurugu, sijui tususie uchaguzi, sijui no nini ile no uchuguzi, naomba niwaambie kitu, Tanzania kuna maisha mazuri sana, unalala na kula hadi kusaza. Kwakifupi ukiwa Tanzania ni kama uko peponi ukikubali kudanganywa na ukadanganyika utajuta. Tanzania ni moja hatuna nchi nyingine, tunapaswa kwa pamoja kuilinda kwa nguvu zetu zote na kukataa kuaminishwe visivyo. Maisha yetu ni ya kipekee na hata Wazungu wenyewe wanayatamani.

Leo nimeona niwaletee simulizi ya safari yangu ya Uingereza ili muone maisha ya huko yalivyo. Nakumbuka ilikuwa Novemba, 2023 ambapo binafsi nilipata Bahati ya kusafari kwenda nchini Uingereza kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Ushirikiano wa Kibiashara kati ya Tanzania na Uingerena uliyofanyika kuanzia tarehe 20 hadi 22 Novemba, 2023. Tulikaa kule kwa muda wa siku 3. Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kusafiri nje ya nchi. Pamoja na jukumu la kushiriki mkutano huo lakini kwangu ilikuwa nafasi adhimu ya kujifunza mambo mengi nje ya Tanzania hasa kupata uzoefu mpya, kuona maendeleo kwa wenzetu, mazingira pamoja na ustaarabu wao.

Tulisafiri kwa ndege ya shirika la ndege la KLM ambayo ilitupeleka hadi Amsterdam, Uholanzi kabla ya kwenda Uingereza. Tulipofika Amsterderm tulisubiri ndege ya kuunganisha safari kwa muda wa saa 4 baada ya hapo tuliendelea na safari ya kuelekea Uingereza. Safari ilikuwa nzuri na yenye utulivu. Na tulipofika Uingereza tulitua katika Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Heathrow kilichopo takriban Kilometa 26 kutoka Katikati ya Jiji la London.

Baada ya kutua, tulipitia hatua kadhaa za uhamiaji ikiwemo ukaguzi wa Hati za kusafiria pamoja na uhalali wa safari husika. Tulipokamilisha taratibu, tulisafiri kuelekea katikati ya Jiji la London kwa kutumia usafiri wa treni wa chini ya ardhi na kisha kutawanyika kuelekea katika hoteli ambazo kila mtu aliweka nafasi kwa ajili ya kufikia.

Nikiwa Jijini London kuna mambo mengi nilijifunza na mengine yalinistaajabisha. Mosi, London hakuna vijiwe vya Tax. Ukihitaji kusafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine yoyote ndani ya Jiji hilo unapaswa ujue wapi unakwenda na ujue pia anuani ya mahali husika unakotaka Kwenda lakini vilevile lazima uwe na ‘’application ya Uber’’ kwenye simu yako kwa ajili ya kuitumia wakati wa kuita usafiri huo pale utakapohitaji kupelekwa sehemu.

Usafiri wa Uber Uingereza ni tofauti kidogo na huu wa hapa kwetu, kule inatumika huduma ya lipia kabla ya kupewa huduma wakati Tanzania unalipia baada ya huduma. Kwahiyo, kwa Uingereza ukiita Uber utapaswa kulipia gharama ya usafiri kabla ya kupewa huduma na Madereva wake ni waaminifu sana, wakipokea hela yako lazima watakuja na watakuja kwa wakati. Kwahiyo unatakiwa muda wote uwe na hela kwenye akaunti yako.

Lakini kitu kingine madereva wa Uber wa Uingereza wanajua kutumia anuani mtandao vizuri, ukiita Uber itakuja palepale ulipo bila kupigiwa simu kuulizwa mara mbilimbili uko sehemu gani na nini ambayo kwa mgeni ingeweza kuwa ngumu kujieleza kutokana na kutojua mazingira halisi alipo kunakosababishwa na ugeni wake.

Unapoita usafiri wa Uber ni muhimu kushika namba ya gari uliyoiita ili itakapowasili uweze kuiona na kuingia. Ikitokea dereva amesimama sehemu tofauti kidogo na kituo ulichopo labda kwasababu sehemu ulipo hakuna sehemu ya kupaki, dereva atakupigia kukujulisha alipopaki na hivyo atakukuomba usogee mbele kidogo au kurudi nyuma kidogo itategemea wapi amepaki. Wazungu wamejaliwa uaminifu ndiyo maana kwenye biashara za kimataifa wanafanya vizuri sana ukilinganisha na sisi Waafrika. Kimsingi uaminifu wao ni waasili ambao umechochewa na malezi yao. Hawana tamaa sisizo na msingi. Siku zote wanaridhika na kile wanachokipata.

Maajabu mmengine niliyoyaona uingereza ni kuwa usiku ulikuwa mrefu kuliko mchana. Saa 12 Jioni jua lilikuwa limeshazama kitambo na kutengeneza giza nene mithili ya giza la saa mbili usiku kwa saa za kwetu Tanzania. Tofauti ya saa kati ya Tanzania na Uingereza ni saa 2. Uingereza iko nyuma kwa saa 2. Ukiwa Uingereza ni kawaida saa 12 jioni kuwa ndani kwasababu usiku unakuwa umeshaingia. Tulizoea kusoma kwenye somo la Jiografia kuwa kuna wakati kunakuwa naa usiku Mrefu kuliko mchana na kuna wakati Mchana unakuwa mrefu kuliko Usiku lakini ukiwa Tanzania huwezi kugundua ni wakati gani usiku unakuwa mrefu kuliko mchana na kinyume chake.

Kitu kingine ni baridi. Mji wa London una baridi kali sana lakini kwa mtu aliyewahi kuishi Makambako, Mafinga, Njombe au Tukuyu hatostaajabu kwasababu baridi ya maeneo hayo inafanana sana na ile ya Uingereza. Lakini kama unatokea maeneo ya Mikoa ya pwani kama vile Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Lindi au Mtwara na ukawa umesafiri kuelekea Uingereza ni muhimu kujihami kwa kubeba makoti ya kutosha.

Tatu, Uingereza huwezi kuwaona traffic barabarani lakini ajabu madereva wanaheshimu sana sheria za barabarani. Taa nyekundi zikiwaka magari yote yaliyopaswa kusimama yatasimama hata kama upande uliyoruhusiwa hauna magari. Vilevile, Uingereza kumetengenezwa njia maalum kwa ajili ya waenda kwa baiskeli na vile kumetengenezwa maeneo maalum ya kupaki baiskeli.

Kitu cha nne nilichojifunza ni kuwa Maisha ya Uingereza ni ghali. Mlo mmoja wa kawaida kwa mfano chipsi kuku ni shilingi 55,000 na chips zenyewe ni zile za kawaida kabisa. Na kuku wanaotumiwa ni wale aina ya broilers siyo kama hawa kuku wetu wa Shinyanga na Singida tuliyoizoea ukiagiza paja unapata paja kweli unakula hadi unasaza.

Ulaya maisha ni magumu sana. Hebu fikiria yale maji ya nusu lita ambayo Tanzania yanauzwa kwa shilingi 500 Uingereza maji hayohayo utauziwa kwa Pound ya Uingereza 1.5 sawa na shilingi ya Tanzania 5,325 kwa mbadalishano wa TZS 3550 kwa Pound 1.

Lakini pili, suala la usafiri Uingereza si rahisi kama Tanzania. Uingereza hakuna Bodaboda, Bajaji wala tax. Kule usafiri wa haraka wanaoutegemea zaidi ni Uber. Daladala zipo na ni nzuri sana. Kwa hapa kwetu unaweza kuzifananisha na daladala za mwendo kasi isipokuwa tofauti ni moja, daladala za Uingereza ni za ghorofa ambazo zinaruhusu abiria kukaa juu na chini na zingine zimekaa kama za kitalii vile ambazo kwa kule juu ghorofani kuko wazi.

Kama ni Mgeni ni ngumu kutumia usafiri huo kwasababu hujui mitaa wala vituo vya kushukia pamoja na kwamba unaweza kuziona zinapita vituoni. Kwahiyo ukijitia kimbelembele na kiherehere cha kutumia usafiri wa daladala hapo kwa makusudi kabisa unataka kujitafutia kupotea kwenye mji wa watu kisha upate tabu. Kwa ujumla suala la Usafiri uingereza ni ghali sana. Kwa mfano kwa siku mimi binafsi nilikuwa natumia hadi Pound 55 kutoka Hoteli kwenda kikaoni na kurudi bila kuongeza mizunguko yoyote ya zaida.

Kwahiyo unalazimika ukienda kikaoni asubuhi kikiisha jioni unarudi Hotelini. Ukijitia kiherehere cha kuzurura mtaani baada ya kumaliza kikao unaweza kujikuta unamaliza bajeti yako. Asubuhi unatumia Pound 26 kwenda kikaoni lakini Jioni ni ghali kidogo utatumia hadi Poundi 29 kurudi Hotelini. Kwahiyo ukibadilisha Pound 55 kwenda kwenye hela ya Tanzania utapata kama shilingi 195,250/=.

Fikiria kutumia 195,250 kama nauli kwa siku! Kiasi cha pesa kinachotumika kama nauli kwa siku ingekuwa hapa Tanzania sijui ni nani angeweza kumudu. Tanzania tuna maisha mazuri sana.

Nakumbuka siku moja tulipata mwaliko wa Kwenda kutembelea Kituo cha Jilojia na Utafiti wa Madini cha Uingereza ambacho kilikuwa kinaitwa British Geological Survey (BGS) ambacho kipo katika mji wa Nottingham, ni umbali wa takribani kilimeta 205 kutoka London ambao kwa Tanzania unakaribia kufanana na umbali wa Dar es salaam na Morogoro. Katika safari hiyo tulitumia usafiri wa treni na tulilpa shilingi 400,000 kwa kwenda na kurudi. Treni tuliyopanda haikuwa nzuri kuzidi treni zetu. Sasa unaweza kuona Tanzania maisha yetu yalivyokuwa rahisi ukilinganisha na treni ya Uingereza.

Unaweza kuona, ukisafiri kwa Treni kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma Matanzania atapaswa kulipa nauli wastani wa shilingi 50,000/= kwa Daraja la uchumi. Unaweza kuona Tanzania kuna maisha mazuri kiasi gani, halafu mniambie nihame Tanzania kwakweli siwezi kuhama hata mnipe nini. Kwa yale maisha niliyoyaona pamoja na kwamba nilipata fursa ya Kwenda kusoma huko, nilisema hapana, kama kusoma nitasoma hapahapa Tanzania kwa Mama yangu Mhe. Dokta Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungono wa Tanzania ambaye kimsingi amefanya mengi katika Sekta elimu na ameboresha miundombinu ya vyuo Vikuu kupitia miradi mbalimbali na kufanya mazingira ya kufundisha na kujifunzia kuwa bora zaidi.

Ukiwa Tanzania ni rahisi kuilaumu Serikali kwa kusema Tanzania kuna miasha magumu lakini ukweli ukitembea utakuja kugundua kuwa maisha yetu ni rahisi sana. Kwa mfano suala la Makazi, kupanga nyumba ya kuishi uingereza kiukweli ni ghali sana. Nilipata nafasi ya kupiga soga na dereva wa Uber aliyenibeba kama mara mbili. Dereva huyo alikuwa Raia wa India aliyeenda Uingereza kwa ajili ya masomo lakini alipomaliza masomo yake aliamua abaki Uingereza na akajiajiri kwenye biashara ya Uber. Alisema Uingereza maisha ni magumu sana na akatolea mfano yeye anapokaa wamechangia nyumba na rafiki yake kwa maana nyumba yao wanakaa familia mbili, kwa maana ya familia yake na familia ya rafiki yake lakini ajabu pango kwa mwezi wanalipa Milioni 4 na nyumba yenyewe ni vyumba 2 na sebule.

Nikawa najiuliza nyumba ya vyumba 2 kwa Dodoma nyumba ya aina hiyo iliyojengwa maeneo ya Msalato ni Shilingi 400,000.00 tu na ukilipa miezi 6 itakuwa jumla shilingi 2,400,000.00. Lakini ukiwa nyumbani kwetu Songea nyumba aina hiyo ya vyumba 2, sebule, na jiko utalipia shilingi 150,000 kwa mwezi.

Lakini sasa kwa uingereza ukiwa Jijini London kwa miezi 6 utalipia jumla shilingi 24,000,000.00. Dereva huyo aliendelea kusema kuwa maisha yake yote anakula mlo mmoja hawezi kumudu mlo zaidi ya mmoja lakini kwetu Tanzania tukunala milo 3 au zaidi. Kila kitu unachotaka kula kipo na bei yake ni chee kabisa.

Uingereza unaweza kujikuta unalipwa mshahara mkubwa lakini wote utaishia kwenye kula, gharama za usafiri, pamoja na kulipia nyumba. Kumbuka pia kuna Kodi. Huwezi kuona uzuri wa Tanzania ukiwa Tanzania, ukitoka utaujua.

Nilikutana na dereva mwingine ambaye ni msomali aliniambia kuwa ukiwa Uingereza ukifanya manunuzi usilinganishe manunuzi kwa fedha za nchi ulikotoka ukifanya hivyo utapata ukichaa kwasababu utajiona unatumia zaidi kuliko kawaida. Nilimwelewa Dereva huyo lakini hata hivyo, sikuweza kutumia bila kulinganisha thamani ya Pound niliyotumia dhidi ya sarafu ya nchi yetu.

Kwa ujumla Tanzania tunaishi vizuri tunakula vizuri, tunalala vizuri, tunasafiri vizuri kutoka sehemu moja kwenda nyingine lakini pia tuna vyakula vya kila aina unachagua wewe ule nini na wakati gani. Amani imetamalaki na unaweza kwenda kokote wakati wowote bila kugubudhiwa na mtu yoyote.

Tuna uhuru wa kuzungmuza, kufanya maamuzi na kushirikishwa katika masuala mbalimbali ya maendeleo. Hii nchi ni nzuri sana, tuna Rais Mzuri, mama mwenye huruma, upendo na kujali. Ni muhimu kila mtu atenge muda kumwombea kama si kwa dhahiri hata kwa siri. Anafanya mengi yenye masilahi na nchi yetu. Tumlipe kwa kumpa kura nyingi. Dhahabu lazima itunzwe kwa maslahi ya nchi.
Umezoea kuiba iba hapa Dar plus uchawa unaona maisha simple. Kwa style hii ukienda kwa hizo nchi lazima uone mateso. Sasa mtu kama wale wabunge uchwara kutoka Zanzibar wanaweza kuishi huko?
 
Serikali inachukulia poa lakini ukweli ni kuwa tatizo la akili nchini ni kubwa sana.
 
Back
Top Bottom