Huwezi kutenganisha Uislam na Uarabu wakati uislam Mwanzilishi na Muenezaji wa dini hiyo alikuwa Mwarabu

Huwezi kutenganisha Uislam na Uarabu wakati uislam Mwanzilishi na Muenezaji wa dini hiyo alikuwa Mwarabu

Na Waarabu Wakristo tunawaweka wapi?

Naweza nikasema kama ifuatavyo;

Hao kulingana na maamrisho ya Yesu anawakaribisha. Maana Yeye anasema hana ubaguzi. Wataendelea kuabudu kwa lugha yao.

Lakini pengine wameona uislam chombo cha kueneza tamaduni, mila na desturi za kiarabu hakiwapi matarajio yao ya kiroho. Zaidi ya kusisitiza mila na desturi zao ambazo si spiritual.

Pia kwao wataonekana wameasi desturi zao. Na ukiwa katika nchi za dunia ya kiarabu lazima ikuletee shida.
 
Naomba ushahidi kuwa Yesu ni Myahudi.

Vitabu vinasema. Na mengi alifanya kulingana na desturi za kiyahudi kama vile kutahiriwa ktk siku ya nane baada ya kuzaliwa.
 
1 unaelewa maana ya ibada kwanza kijana 2 muanzilishi yupi wa uislam alikua muarabu kama unamaanisha s a w basi unakosea sababu uislam haukuanzia kwake 3 qur an kweli imeandikwa kwa kiarabu ila uislamu haukuanzia kwenye qur an vilipita vitabu vingi kabla ya qur an 4 uislam hauna majina maalum kijana la msingi Jina liwe zuri hata happy unaweza ukajiita uislam sio Jina kijana 5 waarabu hakua na utamaduni wa kuvaa kwakujistiri kabla ya ujio wa qur an walikua wanavaa vaa tu hovyo hovyo 6 Majengo ndio nini kijana uislam hauna hizo mambo ndio maana watu wanasali popote pale muhimu pawe Safi tu 7 uislam hauna ibada ya musiki wala nyimbo kijana 8 uislam hauna mapishi ya kiarabu kijana uislamu una ruhusu kula chochote maadam ni halali na kizuri 9 Muziki sio sehemu ya sherehe za waislam kijana acha kupotosha watu 10 kabla ya uislam waarabu walikua hawazikani walikua wanafukiana tuuu mwisho waarabu wasiokua waislam nao tunawaeka upande gani wenyewe

Njoo na uthibitisho mmojawapo wa hoja uluzotoa. Naomba ukafanye homework yako. Nimeandika haya baada ya kufanya research ya muda mrefu. Hivyo ni vyema na wewe uka cite authority kwa kila hoja. Vinginevyo nitaita mazungumzo ya kwenye kijiwe cha kahawa.
 
Tofauti kubwa ya Ukristo na Uislamu ni hii hapa; huwezi kuutenganisha uislamu na uarabu wakati unaweza kuutenganisha Ukristo na Wazungu; tutapata Papa Mwafrika kabla hatujapata Mufti Mzungu

Lusekelo alisema kuzika kwenye masanduku ni utamaduni wa wazungu. Sio dini ya ukristo. Niambie leo hii ni mwafrika gani mswahili anazikwa bila sanduku? Maamuzi yote ya dini ya kikristo hasa ukatoliki unatoka vatcan kwa mzungu. Mzungu wa vatcan ndio anaamua wewe mzaramo wa msanga uzikwe vipi au usizikwe sasa hapo unasemaje? Bikira Maria, Brian Deacon(yesu) wakuchongwa waliojaa makanisani mwenu wote wana rangi nyeupe(wazungu) kama nyie wanaume chongeni weusi kama papa hajawafuta kwenye dhehebu
 
Ukristo kwa logic yako potofu uliianza na Wazungu sio?
Au Una maana ukristo ilianzishwa Nicea (Turkey ya sasa) na Mfalme Constantine mtawala wa Mzungu wa Kirumi ndio maana Xmass imewekwa siku ya kusheherekea uzao wa mungu wa kale wa Kirumi.
Tukuitaje mtu unayezungumzia dini ambayo una Zero knowledge ya philosophy yake zaidi ya kukuita ,(ashakum) mpumbavu?

Waroma nao walichomekea magumqshi mengi sana. Mfano easter na Christmas 🎄, kwenye biblia hakuna. Lkn wenyewe wanasherehekea kwa nguvu balaa.

Hata uislam, Muhammad akajaza madesturi ya kwao uarabuni. Mpaka lugha akaifunga iwe kiarabu. Pengine yeye kwa uelewa wake alidhani uislam utabaki katika dunia ya kiislam. Sasa uislam umepotea njia nje ya dunia ya kiislam. Tutegemee matatizo mengi zaidi
 
Tofauti kubwa ya Ukristo na Uislamu ni hii hapa; huwezi kuutenganisha uislamu na uarabu wakati unaweza kuutenganisha Ukristo na Wazungu; tutapata Papa Mwafrika kabla hatujapata Mufti Mzungu
😆
 
Sasa wao kufuata hizo tamaduni za kiarabu kwako imekuathiri nn kwenye maisha yako?
Kinacho shangaza ni ww kujiona una uhuru wa kufuata tamaduni za kimagharibi ila wakati huo unaona wengine hawana haki ya kufuata tamaduni unazo ziita za kiarabu.

Naheshimu maoni yako. Lakini kuwa na fikira tunduizi siyo dhambi. Na labda ukadhani wewe usiyehoji mambo na kutafakari mambo ni mtakatifu. Haiwezi kuwa hivyo.
Pia jua ya kuwa, magharibi hakuna dini iliyoanzia huko. Dini hizi mbili za ukristo na uislam chanzo ni mashariki ya kati au Asia 🌏 ndogo.

Mwisho muache kusalimiana asalam aleykum, pia muache kutaja yale maneno ya swala tano kwa kiarabu (bali yatamkeni kwa lugha yenu ya eneo husika duniani kote) ili tujue uarabu si kitu katika uislam.
 
lugha ya kiarabu kama ulikuaujui ndio imeuganisha waislam wote duniani kwenye ibada.mkristo akiende jumapili kanisani sehemu ambayo lugha inayo zungumzwa si lugha yake anakuwani mpenzi mtazamajitu.

Sasa wewe hufikiri kwa nini iwe kiarabu na isiwe kihindi au kichina
 
Iko sahihi sana, na hapa ndio watu Huwa wanashindwa kuelewa tofauti ya Uislam na Ukristo.

Kwamba wakati Uislam ni dini yenye basis ya Mila na desturi, Ukristo ni dini iliyobase katika Imani kwa njia ya YESU Kristo.
Dini zote duniani zina basis ya mila na tamaduni fulani

Kama waislam watakavyo kataa dini yao kuwa na basis za mila na tamaduni za kiarabu basi hata wewe pia utakataa dini ya ya Ukristo kuwa na basis ya mila na damaduni za Warumi kwa kiasi kikubwa
 
imetumika lugha moja iliupatikanike wepesi wa kuabudu tofauti na ukristo

Kwa hiyo linguistic environment ya watu wote duniani iko sawa?

Moja ya sababu inayofanya elimu iwe dhaifu Tanzania 🇹🇿 ni lugha ya kufundishia. Ni kwamba mtoto anafundishwa kwa lugha ambayo siyo mama. Hivyo haelewi kikamilifu. Maana akiwa darasani anafundishwa kiingereza, akitoka nje anaongea katika lugha ya mama. Hivyo linguistic environment is not supporting the learning process.
Hilo likoje katika uislam nje ya ulimwengu wa kiarabu? Wote wanaelewa sawa?
 
Back
Top Bottom