Life2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,387
- 4,880
Endeleeni kupumzika kwa amani Watanganyika wenzetu mliopoteza maisha yenu 29 Oct, mkiwa na lengo la kulipigania taifa hili.
Mauaji ya Kimbari kule Rwanda mpaka leo yanakumbukwa.
Mauaji ya halaiki kwa njaa kule Ukraine (Holodomor) kutoka kwa Urusi mpaka leo bado yanakumbukwa, na bado baadhi ya nchi zinaendelea kuyatambua.
Ukatili wa Bashar Al Saad dhidi ya watu wa Syria yanakumbukwa na raia wa Syria mpaka leo.
Na mengineyo mengi, hakuna nchi au mtu atafanya mauaji ya halaiki dhidi ya raia wake au wa nchi nyingine na dunia ikamchekea. Haipo na haitawahi kuwepo.
Leo Putin, Durtete, Charles Taylor...nk. Wanakesi mahakama za kimataifa kwa makosa ya kukatisha uhai wa watu.
Baada ya mauaji ya halaiki 29 October nchini Tanganyika, bado kuna watu wanataka Watanganyika waendelee kuwachekea makatili wale.
Ni ngumu sana mtu ambaye hajazika mtoto wake au ndugu yake, ameishia kuona nguo tu au viatu kuwachekea makatili wale.
Yapo makundi ya watu wanaoendelea kuwatetea makatili wale na kuendelea kugonga cheers 🍻, na hata kuwapongeza kwa kazi ya kishetani waliyoifanya siku ile.
Kumbukeni #Damu ya mtu haipotei kama leo mnatumia bunduki kuwanyamazisha Watanganyika, ipo siku #Haki yao itapatikana tu.
Endeleeni kujisifu na kunywa mvinyo kwa ushetani wenu ule.
Katika Haki mtathibitika mtakua mbali na kuonewa.