Kwa hiyo wewe hapa unapocomment huna la kufanya?
Tusijidanganya Mkuu wa mkoa sijui waziri wote ni binadamu wana vitu wanavipenda kwenye burudani. Kuna wengine wanapenda muziki, bongo movies na wengine mpira wa miguu. Kwa hiyo sishangai mkuu wa mkoa kuongelea hilo swala provided hajaongea kama mkuu wa mkoa ameongea yeye kama yeye binafsi, kwa wakati na mazingira sahihi na husika.
Tusitake kuwadisown viongozi wetu kwenye jamii. Unakuta mtu anasema Makonda anaongelea vitu vya kipumbavu unajiuliza je inamaana hata yeye anafuatilia upumbavu? Kweli unataka kusema wote tuliopo kwenye jukwaa hili ni wapumbavu? Wote tunaocomment hapa ni wapumbavu? Je ingekuwaje kama angekuwa ameongelea simba na yanga? Au mtibwa na Mbeya city? Au Ali kiba na Diamond?
Hao akina Wema na Hamissa ni Socialites mtu yeyote aliyepo mtandaoni na mpenda burudani anawafahamu. Why not Makonda?
Nashangaa watu pia wanaingiza siasa pia hivi mmesahau Wema alivyokamatwa na bangi viongozi wote wa upinzani walikuwa upande wake? Akina Tundu Lissu, Kibatala ndiyo waliokuwa wanakwenda kumtetea? Halafu mahakama ikawa inafurika akina mbowe, Lowassa, Mnyika, Bulaya, Mdee nk? Ilikuwa upumbavu? Mbowe alikuwa anashinda na Wema kama PS wake tushasahau.