Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 13,417
- 23,310
Kwa mtazano wangu kama inawezekana hata TRA ingebinafsishwa tu. Watanzania wanaua wenyewe mashirika yao halafu wanaanza kuwalaumu viongozi.Miaka ya karibuni kumezuka matukio kadhaa kwa serekali kushindwa kuendesha mashirika yake na imepanga kuwapa wageni
Mpaka sahivi mabosi wa mwendokasi wangetakiwa wawe na kesi ya kujibu kwa kushababishia serekali hasara umepewa monopoloy kwenye route na bado inakushinda kwelii
Mashirika ya Tanzania yanakufa kwa sababu mtu anaharibu hapa anahamishiwa kule au hachukuliwi hatua zozote zile za kisheria
Jambo ambalo watu wengi hawajui mzungu au mwarabu anayekuja kama mwekezaji hawezi kuwa na uchungu na Tanzania hata siku moja
Kama serekali imeshindwa kuendesha mashirika yake basi ikubali tu haitaweza kuondoa huu umaskini uliotamalaki hapa Tanzania
Ulaya kupitia ukoloni waliiba rasilimali na wakatengeneza nchi zao na wakaendelea; ile miji mizuri unayoiona ulaya imetokana na ukoloni hasa america kule ndo walivuna kisawasawa
Mfano nchi za saudi arabia baada ya kuvumbua mafuta waliunda shirika lao la aramco kuendesha na kusimamia shughuli zote za uchimbaji wa mafuta matokeo yake aramco lilikua moja ya mashirika makubwa sana dunia yanayoingiza revenue kubwa na hii imepelekea saudi arabia kuendelea sana na kwa mda mfupi
Ukienda qatar, uae rasilimali zao zote zinashikiliwa na makampuni ya serekali njoo nigeria moja ya nchi ambayo ina mafuta mengi utajiri wake wa mafuta iliwakabidhi shell mpaka navyoongea mpaka leo yale maeneo ambayo yapo makampuni ya kigeni yana umaskini wa kufa mtu
Geita kuna mgodi mkubwa sana wa dhahabu lakin hakuna mpact yeyote ambayo geita imepata kutoka na uwepo wa madini
Kama afrika tunataka kuendelea ni kuyaondoa makampuni yote ya kigeni kwa makubaliano ya pande zote ya kuvunja mikataba mbili ili tunufaike na rasilima zetu tofauti na hapo ni uongo
Kuna approach nyingi nchi itatumia ili kuendelea ila njia rahisi ya kuendelea ni kutumia rasilimali zake njia ya kutumia kodi ni ngumu kwa nchi maskini kama Tanzania
Wizi, uzembe tamaa ya mafanikio ya harakaharaka ndiyo iko miongoni mwa Watanzania wengi hata wale wanao join ajira kwa mara kwanza