Huwezi tegemea wawekezaji wa kigeni ndiyo waendeleze nchi

Kwa mtazano wangu kama inawezekana hata TRA ingebinafsishwa tu. Watanzania wanaua wenyewe mashirika yao halafu wanaanza kuwalaumu viongozi.

Wizi, uzembe tamaa ya mafanikio ya harakaharaka ndiyo iko miongoni mwa Watanzania wengi hata wale wanao join ajira kwa mara kwanza
 
Hakuna sheria kali za kuwathibit waizi unategemea nini
 
Tanzania had an experience, tumeshaua mashirika mengi mno, ujinga huo haufai kuurudia tena, mwiko, tusonge mbele!
 
Kwamba kuwapa wazungu na warabu ndo suluhisho
Tulikuwa na mashirika mengi kweli, yoote yaliuwawa, wanapewa wageni kuendesha wakichanganyika na wazawa ili kurithisha uendeshaji sahihi wa shirika husika,wapo waliopewa enzi hizo kwa uaminifu mkubwa WAKAYAUA!
-wape watanzania wasio na ujuzi sahihi, wayaue na waje na visingizio kurasa nzima ya gazeti.
 
Uwekezaji unaleta Maendeleo sema sisi ndio tunajiibia wenyewe ninakumbukuka Barrick walipoingia walikuwa wakitoa Mishahara minono sana Serikali ikawaambia wapunguze kwasababu Watumishi wa Umma wataacha kazi na kuhamia Migodini.
Geita Mine serikali ilikataa wafanyakazi wasilipwe kwa dollar. Wakaona haitoshi wakaanza kukata kodi kila kitu hata allowances ambanzo watumishi wa umma hawakatwi
 
Unatwanga maji kwenye kinu. Kuanzia Mkapa abinasfishe mashirika ya umma inakaribia miaka 30 sasa na bado hakuna ufanisi wowote lakini bado serikali inahangaika kutafuta wawekezaji kutoka nje. Asingekuwa magufuli, ATCL na TRC zilikuwa zimeshakufa kifo cha mende.
 
Tatizo siasa ina nguvu kuliko utalaamu
 
Wazungu wanadanganya sana
Maendeleo sio swala la lelema watu wanaiba mabilion ya fedha za umma maksudi alafu uwachekee ndo maana afrika kuna umaskini wa kutisha

Watu wanaiba wanajua hakuna watakachofanywa
Wamejiwekea kinga wasishitakiwe utawafanya nini na tuna taasisi dhaifu haswa mahakama na bunge fake
 
Ufanisi wa mashirika ya Mkapa upo. Angalia NMB, NBC, TBL, TCC, na mashirika ya Telecoms
 
Magufuli alikuwa akiwatumbua wapuuzi wa mali za uma na kuwasweka ndani mkasema anawaonea! tulieni dawa ya waarabu iwaingie vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…