Huwezi tegemea wawekezaji wa kigeni ndiyo waendeleze nchi

Hakuna Mzungu anakuja Afrika kuwekeza ili awasaidie Waafrika.

Tunaibiwa tu. Fukuza hawa wazungu tuchimbe madini yetu wenyewe. Tukishindwa bora yabaki ardhini vizazi vijavyo vitajua chakufanya
Kama sikosei mwaka jana madini yaliingizia serekali zaidi ya Tzs 600b kati ya hizo contribution ya wachimbaji wadogo ni 40%. Kama wachimbaji wetu wangepata support kidogo mtu, mapato kwa serekali yangelikuwa mara dufu. Hawa wachimbaji wakubwa wanaamisha tu utajiri wetu na watawala wetu - kwa upeo wao - wanaona ndiyo watu wakuletea nchi maendeleo.
 
Hao wakezaji wakubwa ni kuangalia namna ya kuvunja mikataba yao hawana contribution yeyote kwenye nchi

Wanachotuachia ni mashimo alafu wanasema hawapati faida
 
Approach ya magufuli ilikuwa ya hovyo nikuulize swali mwisho wa siku ali-achieve nini
Unajifanya ulikuwa huoni kilichotokea ulikuwa ukimpa hata asante mtumishi wa uma anakataa anakuogopa labda ni mtego.

Ilikuwa ukiingia ofisi ya uma unaulizwa unashida gani nikusaidie! lakini manyang'au yakapita nae acha dozi ya waarabu iingie vizuri imeanzia TPA kule hali ni tete na sasa anaingia DART.
 
Sijaona shida ya wawekezaji, shida ni mikataba mibovu serikali inayojiingiza.

Ukiangalia mkakati wa DP World wanachoenda kufanya ni game changer na kina tija kwa nchi. Lakini huo muda wanaopewa wa kuvuna ndio shida.

Same kwenye madini ndio hayo hayo aiwezekani mtu awekeze $2 billion dollar miaka zaidi ya 30 baadae ana 50% ya economic benefits tena kuipata hiyo share kwa upande wa Tanzania ilikuwa kwa mbinde kweli na bado nchi hiko kwenye disadvantage.
 
Mimi siongei mambo ya watumishi wa umma naongelea uwekezaji
 
Mkuu
Tatizo siyo serikali. Tatizo ni CCM.

Washaanza kuuza nchi vipande vipande. Soon tutauzwa wote
 
Mimi siongei mambo ya watumishi wa umma naongelea uwekezaji
Kwani kinachosababisha kutafuta muwekezaji si baada ya watumishi wameshindwa kuendesha mradi kwa sababu ya rushwa mkuu.

Hivi wangekuwa wangekuwa wanafanya kazi kwa uadilifu wanatoa huduma vizuri unafikiri kungekuwa na haja ya kuleta wawekezaji?
 
kwa hali tulioyonayo ni bora hao wageni, Mpaka tutakofika hatua ya kubadilika tukawa na nidhamu ya kujiongoza ndipo tutaanza kujadili mengine
 
Huu wizi una mahusiano na uongozi. Kama viongozi wapatikana kwa wizi wa kura, unategemea watapata wapi nguvu ya kuzuia wizi? Kama viongozi wangekuwa wapatikana kwa njia halali, wangekuwa na moral authority ya kushughulikia wezi.
 
Tatizo sio ubinafsishaji. Ipo mifano mingi ya wawekezaji wa nje kuchochea maendeleo ya nchi wanakowekeza. China ni mfano mmoja. Tangu walivyoachana na itikadi ya Mao na kuamua kukaribisha makampuni ya Marekani na Ulaya kuwekeza nchini mwao wamepiga hatua kubwa sana ya maendeleo hadi wanaitikisa hata Marekani katika nafasi ya kwanza kiuchumi duniani.

Siri iko kwenye mikataba ya uwekezaji na ufuatiliaji wake. Nchi makini huhakikisha zinapobinafsisha njia kuu za uchumi au kuruhusu uwekezaji kwenye rasilimali muhimu za taifa basi zinakuwa makini sana kujadili na kuingia mikataba itakayohakikisha taifa litapata manufaa yaliyokusudiwa. Pia zinahakikisha zinajijengea uwezo mkubwa wa kitaaluma na kitaasisi kuweza kufuatilia utekelezaji kuhakikisha makubaliano hayakiukwi kijanjajanja.

Tatizo letu wenye dhamana ya kufanikisha hayo wanaona zote hizo ni “fursa za ulaji”. Ndio wakati wa kumiliki mijengo duniani kote, kutembelea magari makali, kufadhili wanyonge kwa sadaka, rushwa na takrima kadhaa na kuwakoga waswahili wenzao mitaani. Wanaachia wawekezaji kila kitu.

Hivyo, ukishakuwa taifa la kitu kidogo, haijalishi. Kubinafsisha na kutobinafsisha yote sawa tu.
 
Ni hatari sana. Kama kitendo cha kusema uwape Mwendokasi wageni ni sawa sawa tu na kuchoma moto akiba ya pesa zako za kigeni. Huo mradi hata serikali ikiamua leo iuendeshe kiufanisi zaidi ya kampuni binafsi inaweza, tatizo ni kuchekeana chekeana.
 
Hao wanaowekea mosi sio wenye uwezo wa kuendesha shirika husika.
Pili dhima Yao sio kuliendesha shirikali Hilo Kwa ufanisi , Bali kuwa chanzo cha mapato Kwa baadhi yetu ili waweze kupata mtaji wao kuwa wawekezaji kwenye hiyo biashara
 
Ila kina KISENA na RIZIMOKO ndiyo wataendeleza? Bora achukue tu MWARABU kila kitu.
 
Kipi cha mswahili kilichofanyika kwa ufasaha.
Mswahili huyu huyu anaeamini ndumba kwenye business ndio aweze endesha uchumi wa nchi.
Africa nzima uchumi unaendeshwa na wahindi au waarabu.
Labda useme wapewe wazawa ambao ni wahindi au waarabu.
 
Hakuna Mzungu anakuja Afrika kuwekeza ili awasaidie Waafrika.

Tunaibiwa tu. Fukuza hawa wazungu tuchimbe madini yetu wenyewe. Tukishindwa bora yabaki ardhini vizazi vijavyo vitajua chakufanya
Madini sio mali yetu sisi ni walinzi TU wao ndio wamiliki Wana KAZI nayo wanapanga bei.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…